Habari za Punde

*MGOSI AWATAKA SIMBA KUSAJILI WACHEZAJI WAZURI NA SIO MAJINA

Na Zainab Nyamka, Dar
Mshambuliaji mkongwe wa Simba SC Mussa Hassan Mgosi amesema, kuelekea katika usajili  wa wachezaji wapya viongozi  wanatakiwa kuangalia wachezaji ambao wanahaki ya kuitetea simba na sio kusajili mchezaji kwa sababu ya jina lake.
Mgosi amesema, Klabu inatakiwa kusajili wachezaji ambao wataipa Simba kile kitu ambacho kinakihitaji ili kuiweka timu katika nafasi nzuri.
Mgosi amesema, wachezaji wa kigeni wanahitajika lakini waangaliwe ni watu gani wanahitajika na wanauwezo wa kuitetea timu kwa akzi watakayoifanya.
"mchezaji wa kigeni anatakiwa kufanya kazi ya ziada ambayo itamzidi yule mchezaji mzawa ili kuweza kuweka utofauti kati ya mchezaji wa kimataifa na mzawa katika klabu,"amesema Mgosi. 
Hilo limekuja baada ya wachezaji wa kigeni wa timu hiyo kucheza chini ya kiwango ukilinganisha na wazawa na wengine kuishia kuishia kukaa benchi.
Mgosi amesema, viongozi wanatakiwa kuangalia makosa yaliyotokea katika msimu uliopita na kupelekea timu kushindwa kufikia malengo ili kuyarekebisha na hata usajili utakapofanyika uwe wa kueleweka.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.