Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana akizungumza na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing mwishoni mwa wiki mjini Dodoma, viongozi hao walijadili masuala mbalimbali ya uwekezaji na ushirikiano.
Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing na ujumbe alioambatana nao wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Dodoma (hayupo pichani) wakati walipomtembelea mkuu huyo wa Mkoa ofisini kwake mwishoni mwa wiki kuzungumzia masuala ya uwekezaji na ushirikiano.
Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing akiagana na Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyohusu masuala ya uwekezaji na ushirikiano yaliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
***************************************
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Mheshimiwa Jordan Rugimbana mwishoni mwa wiki amekutana na Balozi wa China
nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing na kuzungumzia masuala ya kukuza uwekezaji na
ushirikiano baina ya pande hizo mbili.
Mheshimiwa Rugimbana
amemwelezea Balozi wa China kuwa ameunda kikosi kazi cha Masuala ya Uwekezaji
ambacho kina kazi ya kuboresha mazingira ya uwekezaji, kutambua wawekezaji
waliopo na changamoto zinazowakabili na njia bora za kuzitatua kwa lengo la
kuboresha mazingira na kukuza uwekezaji kwenye Mkoa wa Dodoma.
Amesema kwa sasa anataka
kuanzisha eneo maalum la uwekezaji kwenye Mkoa wa Dodoma ambapo kitaundwa kituo
chenye kutoa huduma zote zinazohitajika kwenye uwekezaji na kutakuwa na taasisi
zote zinazohusika na utoaji wa huduma hizo ambapo mwekezaji akifika kituoni
hapo hana haja ya kuondoka kwenda kutafuta huduma sehemu nyingine, mahitaji
yake yote yatatatuliwa hapohapo kituoni na mara moja ataanza shughuli yake ya
uwekezaji.
Pamoja na masuala hayo ya
uwekezaji, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma alimshirikisha Balozi wa China juu ya mpango
wa utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi wa mji mpya wa serikali hapa mkoani
Dodoma wenye lengo la kukamilisha ujenzi wa miundombinu yote muhimu na
kuhakikisha serikali inahamia Makao Makuu Dodoma.
Kwa upande wake Balozi Dkt. Lu
Youqing alimshukuru Mkuu wa Mkoa Dodoma kwa jinsi ambavyo uongozi wake wa Mkoa
ulivyoweka utaratibu wa makusudi wa kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuanza
kushughulikia changamoto zinazowakabili wawekezaji kwa kushirikiana nao na
kusema kuwa anapata taarifa nyingi kutoka kwa wawekezaji wa kichina
wanaoendesha shughuli mbalimbali Mkoani Dodoma juu ya namna ambavyo uongozi wa
Mkoa unashirikiana na wawekezaji hao kutatua changamoto zilizopo.
Vilevile, Balozi wa China
alimhakikishia Mheshimiwa Rugimbana kuwa
atasaidia kuzikutanisha Mamlaka zinazoshughulikia ujenzi wa mji mpya wa
serikali na serikali kuhamia Dodoma na mamlaka ya Manispaa ya Jiji la Beijing
China ambayo inauzoefu na imefanikiwa kujenga mji mpya mbali na ule wa zamani
kwa kipindi cha miaka miwili tu, lengo likiwa kubadilishana uzoefu katika
kutekeleza mradi huo wenye manufaa makubwa kiuchumi hapa Tanzania.
Imetolewa
na:
Idara
ya Mawasiliano ya Serikali
Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa
DODOMA
Mei 30,
2016
No comments:
Post a Comment