Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ally Salum Hapi, akisaini katika kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika moja kati ya Hospitali zilizopo Kinondoni akiwa katika ziara ya utembelea hospitali zote za Kinondoni jijini Dar es Salaam,leomchana.
Leo Jumatatu ya 30/05/2015 Mhe. Hapi, alianza Ziara Kutembelea Hospitali 48 za Serikali zilizopo Wilaya ya Kinondoni. Aidha ziara hiyo inatarajia kukamilika jumamosi ya wiki hii ambapo atatembelea Zahanati na Vituo vya Afya ili Kujionea Huduma na Changamoto mbalimbali zinazo kabili Hospitali Hizo.
Kwa leo Mh DC alitembelea Vituo Vifuatavyo.
1. ZAHANATI YA WAZO
2. ZAHANATI YA MADALE
3. DISPENSALI YA MBOPO
4. ZAHANATI YA TEGETA.
5. ZAHANATI YA KUNDUCHI
6. DISPENSALI YA SALASALA.
7. DISPENSALI YA NDUNBWI.
Akikagua maeneo ya Hospitali, Kote huko Mkuu wa Wilaya alizungumza na Waganga Wafawidhi wa Hospitali, Manesi, Pamoja na Baadhi ya Wagonjwa.,ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ally Salum Hapi, kesho Saa 5 asubui anatarajia kuendelea na Ziara yake.





No comments:
Post a Comment