Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na
wakandarasi nchini wakati wa ufunguzi wa
mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) ambapo
aliwataka makandarasi wazawa kuwa wazalendo na nchi yao ikiwemo kuepuka vitendo
vya rushwa katika maeneo ya Kazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wageni na watendaji wa serikali
wakati akiwasili katika hafla ya uzinduzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa
Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).
Kaimu
Msajili kutoka Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) Rhoben Nkori akiongea
wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya
Usajili ya Makandarasi (CRB)na kuahidi kuendelea kuwapa kipaumbele makandarasi
wazawa na kukabiliana na changamoto zinazowakabil.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) Mhandisi Consolata Ngimbwa akiongea na
wakandarasi(hawapo pichani) ambapo aliwataka makandarasi wazawa kufanya kazi
kwa weledi na kusisitiza kuwachukulia hatua kali za kisheria kwa makandarasi
wenye nia ya kuwakwamisha.
Waziri
wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na
wakandarasi nchini wakati wa ufunguzi wa
mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) ambapo
aliwaahidi makandarasi nchini kuwasimamia kikamilifu na kuwapa fursa na kazi
mbalimbali za ujenzi nchini.

wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea baadhi
ya mabanda wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya
Usajili ya Makandarasi (CRB).

No comments:
Post a Comment