Na
Daudi Manongi, MAELEZO, Dar
es Salaam
HALMASHAURI za Miji
na Wilaya nchini Miji zimekumbushwa kukamilisha zoezi la upatikanaji wa
madawati kwa shule za msingi na sekondari ifikapo juni 30 mwaka huu ili
kutekeleza agizo lililotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Rai hiyo imetolewa leo na
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Rebecca Kwandu wakati wa mahojiano na mwandishi
wa habari hizi kuhusu uchakavu wa madarasa na ukosefu wa madawati unaozikabili
shule za kinesi A na B zilizopo wilaya ya Rorya mkoani Mara.
“Suala la upungufu wa
madawati na uchakavu wa madarasa ni changamoto ya kitaifa na kwamba
lilishatolewa agizo na mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kuhusu halmashauri
zote nchini kuhakikisha ifikapo Juni 30 mwaka huu kila mwanafunzi anaketi
kwenye Dawati” Alisema Kwandu.
Kwa mujibu wa Gwandu alisema
Serikali ya awamu imepania kuinua kiwango na ubora wa elimu nchini kupitia
mikakati na sera ya elimu bure nchini kote.
Aliongeza kuwa hatua
hiyo imeibua changamoto kubwa kwa wanafunzi wengi kujitokeza kwa asilimia kubwa
na hivyo ni wajibu wa halmshauri hizo kukidhi mahitaji ya madawati ili wasome
katika mazingira mazuri.
“Mpaka sasa Serikali
imeendelea kutoka pesa kwa ajili ya elimu bure nchini kote na kumekuwepo kwa
changamoto mbalimbali kama upungufu wa walimu,madawati na madarasa ambapo serikali
inafanya jitihada za kila namna ili kutatua changamoto hiyo”
Akifafanua zaidi
Gwandu alisema Serikali inaandaa harambee mbalimbali na kuongeza wigo wa utoaji
wa vibali vya kuchangia maendeleo ya elimu kwa hiari ili kutoa nafasi kwa wadau mbalimbali wenye nia ya
kufanya.

No comments:
Post a Comment