Habari za Punde

*WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKAGUA MRADI WA MABASI YA MWENDO KASI JIJINI DAR LEO

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akizungumza na mwanafunzi Amina Abdallah wa darasa la sita katika shule ya msingi ya Ukombozi jijini Dar es salaam ambaye amepanda basi la Mwendo Kasi Ajentina na kushuka Manzese, Waziri Mkuu Majaliwa ametumia usafiri wa DART leo kutoka Feri kwenda Kimara Mwisho wakati alipokagua miundombinu ya usafiri huo ili kujionea mafanikio na changamoto mbalimbali zinazojitokeza mara baada ya mradi huo kuanza mwezi mmoja uliopita ili ziweze kurekebishwa na kuuboresha zaidi. 

Usafiri wa DART umekuwa mkombozi kwa wasafiri wengi wa jiji la Dar es salaam wakati wanapotoka majumbani mwao na kuelekea kazini na kurejea majumbani mwao. Katikati ni Bw. David Mwaibula aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Usafiri wa Daladala Dar es salaam (DRTLA) aliyeambatana na Waziri Mkuu kukagua mradi huo leo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akifurahia jambo wakati Mkurugenzi wa DART Bw. David Mgwasa akisamimiana na Bw. David Mwaibula aliyekuwa Mwenyekiti Mamlaka ya Usafiri wa Daladala Dar es salaam (DRTLA) zamani aliyeambatana na Waziri Mkuu kukagua mradi huo leo.
Baadhi ya abiria wakisafiri pamoja na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa kwenye basi la DART.
Moja ya Basi likiwa katika ruti yake kutoka Kimara kuelekea Posta.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akikagua kituo cha Kimara Mwisho mara baada ya kuwasili kituoni hapo
Moja ya basi la Mwendo kasi likipakia abiria katika kituo cha Kimara Mwisho leo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza na mwanafunziambaye jina lake halikufahamika mara moja wakati alipofika kwenye kituo cha mabasi ya Mwendo kasi Kimara Mwisho leo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.