Habari za Punde

*DIRISHA LA USAJILI LAFUNGWA, TIMU KADHAA ZASHINDWA KUWASILISHA USAJILI

Dirisha la usajili kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza la StarTimes na Ligi Daraja la Pili msimu wa 2016/2017 lilifungwa saa 6.00 usiku wa Jumamosi Agosti 6, 2016.

Hadi dirisha linafungwa, timu kadhaa hazikuwasilisha kabisa usajili wake licha ya kukumbushwa kwa njia mbalimbali na uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). 

Akizungumza na mtandao huu, Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas, alisema kuwa Dirisha la usajili wa Ligi Kuu Bara, Daraja la kwanza na la pili limefungwa usiku wa saa sita jumamosi, lakini hadi dirisha linafungwa bado kuna baadhi ya timu zilishindwa kuwasilisha usajili wake.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.