Kikosi kipya cha kwanza cha Simba.
Kikosi cha AFC Leopards.
Keki ya sherehe za kutimiza miaka 80 ya tangu kuanzishwa kwa Klabu ya Simba.
Baadhi ya Viongozi wa Simba wakikata keki.
Mohamed Dewji,akimlisha Keki Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Kikosi cha AFC Leopards.
Keki ya sherehe za kutimiza miaka 80 ya tangu kuanzishwa kwa Klabu ya Simba.
Baadhi ya Viongozi wa Simba wakikata keki.
Mohamed Dewji,akimlisha Keki Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, paul Makonda, akisalimiana na wachezaji wa Simba wakati wa utambulisho wa wachezaji hao katika Tamasha la Simba Day leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika Tamasha hilo Simba walicheza mchezo wa kirafiki na AFC Leopards ya nchini Kenya na kuwatandika mabao 4-0.
**********************************
Na Ripota wa Sufianimafoto, Dar
KLABU ya Simba leo imesherehesha miaka 80 tangu kuanzishwa kwake sambamba na sherehe za Tamasha lao maarufu la utambulisho wa wachezaji wapya ‘Simba Day’ katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika Tamasha hilo mbali na kupambwa na burudani mbalimbali pia Simba ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi yake na AFC Leopards ya Kenya na kuwatandika jumla ya mabao 4-0.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, na Rais wa Simba Evance Aveva, wakiwasalimia mashabiki wa Simba wakati wakiingia uwanjano hapo.
*********************************
Bao la kwanza la Simba lilifungwa na Ibrahim Ajib, katika dakika ya 38 akimalizia pasi nzuri ya Jonas Mkude kwa shuti la umbali wa mita 25 huku akifunga tena bao la pili katika dakika ya 55 akimalizia kazi nzuri ya Mavugo.
Kipindi cha pili Simba ilifanya mabadiliko kwa kuwaingiza Muzamir Yassin, Jamal Mnyate na Laudit Mavugo ambao waliingia na kasi mpya na kuweza kuwatawala AFC Leopards kwa kiasi kikubwa huku wakifika langoni kwa wapinzani wao mara kadhaa.
Bao la tatu lilifungwa na Shiza Kichuya katika dakika ya 66, huku bao la kufungia pazia likifungwa na mshambuliaji mpta kutoka Burundi, Laudit Mavugo, akimalizia kazi nzuri ya mfungaji wa baola tatu,Shizza Kichuya.
Sehemu ya mashabiki wa Simba wakishangilia wakati wa utambulisho huo.
Paul Makonda akizungumza katika Tamsha hilo
Uwanja ulipendeza kiasi chake,......













No comments:
Post a Comment