Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua mashine ya Utla Sound wakati akiwa katika ziara yake Mkoani Katavi ya kukagua shughuli za utoaji wa huduma za Afya na kutathimini shughuli za maendeleo zinazofanywa na wananchi wenyewe kwa kushirikiana na Serikali.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwaonesha nembo ya MSD GOT inayotambulisha kuwa Dawa hiyo inatolewa na Serikali kwa wananchi. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua moja kati ya Friji ya kuhifadhi Dawa za chanjo
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa ndani ya duka la Dawa la MSD kufanya ukaguzi juu ya upatikanaji wa Dawa zote, Kulia ni Mfamasia wa duka hilo Bahati Kazimili
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na mgonjwa katika wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Manispaa Mpanda wakati akiwa katika ziara yake Mkoani Katavi ya kukagua shughuli za utoaji wa huduma za Afya, Kulia ni Mganga Mkuu Manispaa ya Mpanda Dkt. Mahenge
Naibu Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile
akifuatilia taarifa ya dawa katika Bin card kwenye chumba cha uhifadhi dawa
kituo cha Afya Kanoge.
*********************************************
Na WAMJW. KATAVI.
Naibu Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsioa,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile amewataka
wananchi kutumia nguvu kazi yao katika
ujenzi na uboreshaji wa Zahanati katika Wilaya zao kuliko kupeleka pesa nyingi
kwa wakandarasi.
Dkt.Ndugulile ameyasema hao
wilayani hapa wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za utoaji huduma za afya na
kutathimini shughuli za maendeleo
ikiwemo ya upanuzi wa miundombinu zikiwemo ya Zahanati
Alisema kutumia nguvu kazi
zao itasaidia kwa kiasi kikubwa
kupunguza gharama ambazo zingeweza kujitokeza kama wangetoa tenda hiyo kwa
wakandarasi.”Nyinyi ndio wasimamizi wakuu wa shughuli hizi na mkiharibu
tutakuja kuwalaumu nyinyi
Aidha,alisema Serikali imetoa
shilingi milioni 400 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya huduma za afya nchini
kwa upande wa uzazi wa dharura ikiwemo upasuaji, wodi ya wazazi,maabara
,wodi ya watoto pamoja na nyumba ya mtumishi kwenye vituo vya afya ambapo
ujenzi huo unaanza mara moja
Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile
ameendele kuwatoa hofu wananchi juu ya hali ya upatikanaji wa dawa, huku
akiwasisitiza wananchi wasiuziwe dawa zozote muhimu kwani hali ya upatikanaji
wa Dawa ni nzuri maeneo yote na sasa ni wastani wa asilimia 80.
“Katika kituo cha Afya Kanoge, bajeti
ya dawa imeongezeka kutoka Milioni 300 mpaka Bilioni 2.5, kwahiyo dawa tunazo
za kutosha, hivyo hatutarajii kuona mtu aje hapa aambiwe akanunue dawa sehemu
nyingine, wamenithibitishia waganga wangu asilimia 90 ya dawa muhimu zipo”
aliendelea Dkt. Ndugulile
Wakati huo huo Dkt. Ndugulile amesisitiza
watumishi wa afya juu ya utunzaji wa kumbukumbu za dawa katika stoo ya madawa
ikiwemo kuweka za kujua idadi za dawa zilizoingia na kutoka pamoja na utunzaji
wa takwimu za mahudhurio ya wagonjwa wa kila siku, jambo linalopunguza ufanisi
katika kazi.
Hata hivyo Dkt. Ndugulile amemtaka
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Mpanda Dkt. Mahenge kuanzisha ofisi ya kushughulikia
malalamiko ya watu pindi wanapokutana na changamoto wakati wakipata huduma
katika Kituo hicho cha Afya.
Naye
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Yahaya Hussein wakati
akiwasilisha taarifa ya Mkoa alisema kuwa Mkoa wa Katavi unakabiriwa na uhaba
mkubwa wa watumishi wa kada ya Afya hali inayopelekea changamoto kubwa katika
utoaji wa huduma kwa wananchi.
“Hadi kufikia Septemba 2017
Mkoa wa Katavi una jumla ya watumishi 693 sawa na asilimia 28 kati ya watumishi
2,437 wanaohitajika, kati ya hao 19 ni watumishi ngazi ya Mkoa na 674 ngazi ya
Serikali za mitaa, kwa ujumla Mkoa wa Katavi una jumla ya upungufu wa watumishi
1,744” Alisema Dkt.
Hussein.
Dkt.
Yahaya Hussein aliongeza kuwa Mkoa unaendelea kuzisimamia Halmashauri
kuhakikisha zinatenga bajeti kwa ajili ya kuwakatia kadi za Afya ya Jamii (CHF)
wazee ili kuendelea kupata Huduma za Afya kwa urahisi katika maeneo yao.
Mpaka kufikia Mwezi Septemba
2017 jumla ya wazee 19,248 wametambuliwa, na kati ya hao jumla ya wazee 1,807
sawa na asilimia 9.4 wameshapatiwa kadi za CHF katika Halmashauri zote za Mkoa
wa Katavi.







No comments:
Post a Comment