Naibu Waziri Ofisi ya Makamu
wa Rais Mh. Kangi Lugola akisalimiana na Uongozi wa Mamlaka ya maji Safi na
usafi wa Mazingira mjini Dodoma (DUWASA) alipofanya ziara ya kutembelea Ofisi
hizo mjini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Kangi Lugola akifafanua jambo alipokua akiongea na Wafanyakazi wa Mamlaka ya maji Safi na usafi wa Mazingira mjini Dodoma (DUWASA) mjini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Kangi Lugola akielekeza jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji Safi na usafi wa Mazingira mjini Dodoma (DUWASA) David Palangyo wakati wa ziara ya kutembelea mabwawa ya kuhifadhi maji taka yanayotumiwa na DUWASA katika eneo la Swaswa mjini Dodoma. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Kangi Lugola akiwa pamoja na Ujumbe toka DUWASA akikagua mabwawa ya kuhifadhi maji taka katika eneo la Swaswa na Ilazo mjini Dodoma ambapo alifanya ziara.
Sehemu ya mabwawa ya kuhifadhia maji taka inayotumiwa na Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira mjini Dodoma (DUWASA) katika eneno la Swaswa.
******************************************************
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu
wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola hii leo amefanya ziara ya
kushtukiza katika Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma
(DUWASA) ikiwa ni pamoja na kutembelea miundombinu ya Mamlamka hiyo.
Waziri Lugola amesikitishwa
na namna Mamlaka hiyo ilivyoshindwa kuhimili kiasi cha maji taka yanayozalishwa
katika Mji huo wa Dodoma na kutitiririka katika
makazi ya watu bila kutibiwa (Treated).
Katika ziara hiyo Naibu
Waziri Kangi Lugola ameitaka Mamlaka hiyo kuja na mpango wa haraka wa kudhibiti
maji hayo kwa lengo la kudhibiti usafi wa Mazingira na Ustawi wa Wananchi.
“DUWASA mmekuwa mkitiririsha maji taka bila kuyatibu kwenye makazi ya watu, na
kwenye kilimo cha mpunga, na mmepelekea baadhi ya watu kuyahama makazi yao.”
Lugola alisisitiza.
Aidha Waziri Lugola ameitaka
DUWASA kuhakikisha mabwawa mawili yaliyotelekezwa eneo la Swaswa yanakarabatiwa
ili kuhimili kiwango cha uharibifu wa mazingira kabla ya tarehe 31/12/2018, na
kuwataka kuimarisha ulinzi kuzunguka mabwawa yote ili watu wasichepushe maji
katika mashamba yaliyopo pembezoni mwa mabwawa hayo.
Katika hatua nyingine, Naibu
Waziri Lugola ameitaka Mamlaka hiyo ya DUWASA kutumia gari ya matangazo na
kushirikiana na viongozi wa Serikali za mitaa kutoa elimu kwa wananchi wa
maeneo hayo juu ya athari ya matumizi ya maji hayo machafu
DUWASA pia imetakiwa kupata
kibali kutoka kwa Mamlaka ya Bonde la Maji ya Wami-Ruvu cha kutiririsha maji
taka kwenye mazingira na kuhakikisha maji hayo yanatibiwa kwa kiwango kinachoruhusiwa
kwa mujibu wa sheria na kufanya Tathmini ya Kimkakati ya Mazingira kuendana na
ongezeko la watu.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa
DUWASA Bw. David Pallangyo amesema kuwa walipokea mabwawa hayo kutoka kwa iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji
Makao Makuu (CDA) mwaka 2002 na kukiri kutiririsha maji hayo bila kuyatibu
katika mazingira.
Bw. Palangyo amebainisha
kuwa Ofisi yake ina mkakati wa muda mrefu wa kujenga mabwawa makubwa zaidi eneo
la Nzuguni ili kukidhi mahitaji ya sasa na kuendana na ongezeko la idadi ya watu
baada ya Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi.
No comments:
Post a Comment