Na Amina Kasheba, Dar
MWANAMUZIKI Papii
Kocha hatimaye ameanza kuachia madini yake aliyokusanya kwa kipindi cha miaka
13 iliyopita akiwa jela kwa kuachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la
Waambie.
Akizungumza
na mwandishi wa mtandao huu, Papii Kocha amesema kuwa amenza na kibao hicho
chenye ujumbe kwa wanadamu ili kuikumbusha Jamii kutokata tamaa katika maisha
ilimradi tu wamejaaliwa pumzi.
Aidha
amesema kuwa lengo la kuanza na wimbo huo ni kuwafanya watu wamkumbuke mungu
kwa lolote wanalofanya hapa duniani na pindi wanapopatwa na majaribu ama
mitihani ya kidunia katika harakati za maisha wasikate tamaa kwamwe.
‘’Inabidi
waamini kuwa kila jambo hupangwa na mungu na kwa malengo na makusudi yake
ambayo sisi wanadamu hatuwezi kujua ya kesho ni yapi baada ya kupatwa na
maswahibu’’ alisema Papii
Papii alisema
kuwa japo kwa sasa kuna ushindani mkubwa katika soko la muziki lakini anaamini atafanya
vizuri ili kuendana na soko hilo ambalo kwa sasa linazidi kuchechemea na
kuwaachi njia vijana wa Bongo Flava watambe.
“Nimerudi kufanya kazi tena ili kurudisha
adhi ya muziki wa dansi kama ilivyokuwa kama enzi za wimbo wangu wa Seya,
naamini mashabiki zangu na watanzania kwa ujumla watanipokea ili niweze
kuusongesha muziki wa dansi kama nilivyopanga. Alisema Papii
No comments:
Post a Comment