Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza
kushoto) akitoa ufafanuzi wa idadi ya waandishi watakaohitajika katika mkutano
wakati wa mkutano wa majadiliano na Rais
wa Shirikisho la Mipira wa Miguu Duniani (FIFA) Bw.Gianni Infantino utakaofanyika
mnamo Februari 22, Mwaka huu na waandishi wa habari, katika mkutano wake na
Wahariri wa Habari za Michezo (hawapo pichani) nchini leo jijini Dar es Salaam,Katikati
ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi Suzan Mlawi na Kulia
ni Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw.Wilfred Kidau .
Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bw.Wilfred Kidau akitoa ufafanuzi kuhusu ajenda za mkutano wa Rais wa Shirikisho la Mipira wa Miguu Duniani (FIFA) na CAF utakaofanyika nchini Februari 22,2018 katika mkutano na Wahariri wa Habari za Michezo nchini (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa Habari kutoka Gazeti la Nipashe Bi Somoe Ng’itu akiuliza swali kuhusu utaratibu wa waandishi wa habari watakaofika Ikulu kuripoti tukio la Rais wa Shirikisho la Mipira wa Miguu Duniani (FIFA) kukutana na viongozi wakuu wanchi, kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani ) leo jijini Dar es Salaam katika mkutano wa wahariri wa habari za michezo nchini.
************************************************
Na
Anitha Jonas – WHUSM, Dar
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Duniani (FIFA) kufanya mkutano wa
majadiliano na vyombo vya habari kumi na mbili vya ndani ya nchi.
Taarifa
hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe katika mkutano na wahariri wa habari za michezo
uliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
‘’Huu
ni utaratibu wa viongozi wa FIFA kufanya mkutano wa mazungumzo na waandishi wa vyombo
vya habari katika nchi wanazofanyia mikutano yao ya kikazi kama ulivyo mkutano huu wanaotarajia
kuufanya nchini Februari 22,mwaka huu,’’alisema Dkt. Mwakyembe.
Akiendelea
kuzungumza katika mkutano huo Waziri Mwakyembe alieleza kuwa Rais wa FIFA Bw.
Gianni Infantino anatarajia kuwasili nchini alfajiri ya saa nane usiku kuamkia Februari,
22 2018 ambayo ndiyo siku ya mkutano na saa tatu asubuhi yake ataelekea ikulu
kukutana na viongozi wakuu wa nchi.
Naye
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Bw.Wilfred Kidau alitoa
ufafanuzi kuhusu mkutano huu wa viongozi wa FIFA na CAF kuwa umebeba ajenda
mbalimbali ikiwemo kujadili kuhusu Maendeleo
ya Soka la Wanawake,Maendeleo ya Soka la Vijana,Utaratibu wa kusaidia Vilabu
vya soka pamoja na vipaumbele mbalimbali vya kukuza soka kwa nchi za Afrika.
‘’Mkutano
huu wa FIFA unatarajia kufanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini
Dar es Salaam (JNICC) na ni sawa na kikao cha ndani ambacho kimelenga zaidi
kujadili masuala ya maendeleo ya shirikisho hilo kwa ajili ya kuandaa agenda za
mkutano mkuu wa FIFA wa dunia hivyo ombi kwa waandishi wa habari ni kuelewa
dhana ya mkutano siyo kuwa wamenyimwa fursa bali huo ndiyo utaratibu’,’alisema
Bw. Kidau.
Pamoja
na hayo Bw.Kidau alifafanua kuwa miongoni mwa vyombo vitakavyopata fursa ya
kushiriki majadiliano hayo baadhi yao watarusha mazungumzo hayo mbashara katika
vyombo vyao hivyo wadau wengine wataweza kufuatilia tukio hilo moja kwa moja
kupitia vyombo hivyo.
Halikadhalika
Rais huyo wa FIFA anatarajia kuondoka nchini jioni mara baada ya kumaliza
mkutano mwake na kushiriki chakula cha jioni.
No comments:
Post a Comment