Na Mwanaheri
Masoud, Dar
Nguli wa
mitindo barani Afrika ,Mustafa Hassanali amealikwa katika hekalu la Buckingham Februar
19 mwaka huu kwa shughuli ya
kubadilishana mawazo kuhusu mitindo kwa nchi za jumuiya ya madola.
Hassanali
atakuwa ni miongoni mwa wageni wabunifu wengine wa Kimataifa walioalikwa kimataifa
kutoka nchi mbalimbali, huku wakisherehekea shughuli ya kifahari inayohusu
mitindo ,katika hekalu la malkia wa Uingereza queen Elizabeth, na kufurahia ubora
wa kazi za ubunifu.
“Ni heshima
kubwa na ufahari kupata mwaliko huu kutoka kwa Malkia ili kuhudhuria sherehe ya
kazi za mitindo kutoka nchi zote za jumuiya ya madola ,hii inaonyesha kuwa kazi
zangu zinatambulika kitaifa na kimataifa na kujitolea katika sekta ya mitindo
ya Tanzania inakubaliwa na kutambuliwa’’ amesema Hassanali
Katika
safari hiyo mwanamitindo huyo amepata udhamini katika Shirika la Ndege la
Rwanda ambapo atasafiri kutoka Afrika hadi mji wa Gatwick nchini Uingereza
kupitia ndege yao ya moja kwa moja A330-300.
“Ni heshima
kubwa na tunajivunia kuweza kumsafirisha nguli wa mitindo Mustafa Hassanali
aweze kuhudhuria sherehe ya mitindo iliyoandaliwa kwa nchi za jumuiya ya
madola.”amesema Meneja wa Rwanda Air nchini Tanzania , Ibrahim Bukenya .
Katika hafla
hiyo ya kubadilishana mawazo kuhusu mitindo kwa nchi za jumuiya ya madola, inatarajiwa
kuhudhuriwa na wabunifu 52 na wataalam wa sanaa za mikono kutoka nchi tofauti
za jumuiya ya madola , ambao wataungana kutengeneza nguo moja ya kipekee na
endelevu ,ambayo itaonyeshwa kwenye sherehe hiyo.

No comments:
Post a Comment