Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na wadau wa ngumi (hawapo pichani) kuhusu mchakato wa kukamilisha rasimu ya katiba ya kusimamia mchezo wa ngumi nchini maara baada ya kukabidhiwa jana jijini Dar es Salaam,kulia kwake ni Msajili wa Vyama vya Michezo Nchini kutoka Baraza la Michezo la Taifa Bw. Ibrahim Mkwawa.
Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa Bw.Mohamed Kiganja (kulia) akitoa taarifa kuhusu mchakato wa kuundwa kwa rasimu ya katiba ya mchezo wa ngumi kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) kabla ya makabidhiano ya rasimu hiyo jana jijini Dar es Salaam,wapili kulia ni Msajili wa Vyama vya Michezo Nchini kutoka Baraza la Michezo la Taifa Bw Ibrahim Mkwawa
Mwenyekiti wa Kamati ya Kuunda rasimu ya Katiba ya kusimamia mchezo wa Ngumi nchini Bw.Emmanuel Salehe akikabidhi rasimu ya katiba hiyo kwa Mheshimiwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe () jana jijini Dar es Salaam katikati ni Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa Bw.Mohamed Kiganja.
*******************************************************
Na
Anitha Jonas – WHUSM, Dar
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameipongeza Kamati
iliyoandaa rasimu ya katiba ya mchezo wa ngumi nchini kwa kumaliza kazi hiyo
kwa wakati.
Mheshimiwa
Mwakyembe ametoa kauli hiyo alipokuwa akikabidhiwa rasimu ya katiba hiyo jana
jijini Dar es Salaam mara baada kukamilika kwa kuandaliwa kwake na kamati
maalum iliyokuwa na wajumbe 13 wakuteuliwa ambao walifanya kazi ya kuzunguka
kwa wadau wa ngumi na kukusanya maoni. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
“Nitateuwa
watu wasaba kutoka katika kamati hii iliyounda rasimu watakao uungana na Baraza
la Michezo la Taifa kuboresha rasimu hii ili tuweze kuitisha kikao kikubwa cha
wadau wote wa mchezo wa ngumi na tuweze kuipitisha rasimu hii,”Dkt.Mwakyembe.
Akiendelea
kuzungumza katika makabidhiano hayo Waziri Mwakyembe alieleza kuwa ataendelea
kupokea maoni ya wadau hao ndani ya miezi mitatu kwa kuzingatia sheria ili
kufanikisha kikao cha kupitisha rasimu hiyo ambacho kitaitishwa kwa mujibu wa
sheria ili kufanikisha lengo la kuboresha sekta ya mchezo wa ngumi nchini.
Pamoja
na hayo waziri huyo alisisitiza kuwa na mapema wiki ijayo atamuagiza Katibu Mtendaji
Baraza la Michezo la Taifa Bw.Mohamed Kiganja kutangaza wajumbe atakao kuwa amewateuwa
kuungana na BMT katika kuboresha rasimu hiyo.
Akizungumza
katika sherehe za makabidhiano ya rasimu hiyo ya katiba ya kusimamia mchezo wa
ngumi nchini Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw.Emmanuel Salehe alieleza kuwa pamoja
na kukamilisha rasimu hiyo kamati hiyo iliunda pia kanuni za kusimamia mchezo
wa ngumi kwa lengo la kuhakikisha misingi imara inawekwa katika kuboresha sekta
ya mchezo huo.
Kwa
Upande wa Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja
alisema kuwa ofisi yake iko tayari kuungana na wajumbe watakaoteuliwa na
Mheshimiwa Waziri kukamilisha mchakato wa kuboresha rasimu hiyo kabla ya
kupitishwa.
Pamoja
na hayo naye bondia wa zamani aliyekwisha kushinda katika mikanda ya kimataifa
Bw.Rashid Matumla alitoa maoni yake pamoja na kuipongeza serikali kwa kufanya
maamuzi ya kuunda chombo imara kitakacho simamia mchezo wa ngumi kwa kuzingatia
sheria tofauti na awali huku akiwasihi wadau wangumi kuacha tofauti zao na
kuangalia suala la msingi kuboresha mazingira ya mchezo huo na kuufanya uwe na
tija kwa zaidi pamoja na kuondoa mazingira yenye utata katika uendeshaji wa
mchezo huo.
Mmoja wa wanakamati waliyoandaa rasimu ya Katiba ya kusimamia mchezo wa ngumi Bw.Ally Champion akitoa maoni yake na kuwasihi wadau wangumi kuacha tofauti zao za vikundi vyao waungane kwa lengo la kuimarisha mchezo wangumi kwa taifa jana katika mkutano wa kukabidhi rasimu hiyo kwa Mheshimiwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani).
Baadhi ya wajumbe waliyoandaa rasimu ya Katiba ya kusimamia mchezo ngumi wakiwa katika picha ya pamoja na Mheshimiwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (wanne kulia)mara baada ya kumkabidhi rasimu hiyo jana jijini Dar es Salaam,watatu kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kuunda rasimu hiyo Bw.Emmanuel Salehe na watatu kulia ni Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa Bw.Mohamed Kiganja.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto)
akimsiliza bondia wa kike Bi.Feriche Mashauri (kulia) alipokuwa akimweleza changamoto
za mchezo wa ngumi nchini jana jijini Dar es Salaam baada ya Waziri
kukabidhiwa rasimu ya mchezo wa ngumi .
No comments:
Post a Comment