Na Amina Kasheba
MWANAMITINDO maarufu nchini, Asya Idarous
amepewa tuzo ya mwamitindo bora.
Tuzo hiyo
alipewa marchi 8 mwaka huu na kampuni ya Life Achievement kama mwanamitindo ambaye anayebuni mavazi mbalimbali na
kusaidia vijana katika sekta hiyo.
Asya Idarous alitangaza kustaafu mwenzi uliopita na kubaki kama mshauri katika jukwaa
la Lady in Red na kwa wanamitindo mbalimbali.
Akizungumza
na mwandishi wa mtandao huu jijini Dar es salaam, Asya, alisema amefurahi kupewa tuzo hiyo
kwani ni heshima na kutambua kile anachokifanya pamoja na kutoa fursa kwa
vijana.
“Nimefurahi
sana na napenda kuwashukuru sana waandaaji wa tuzo hii na wale wote walioniwezesha mimi kupata
tuzo hii, kwani wameona umuhimu katika tasnia ya mitindo,” alisema Asya.
Hata hivyo
asya idarous aliwaomba wanamitindo wawe wabunifu katika kuandaa mavazi haswa nchini kwa lengo la kuitangaza nchi na kukua kimaendeleo.

No comments:
Post a Comment