Na Mwanaheri
Masoud, Moshi
KAMPUNI ya
Rock-explorer ya mkoani Kilimanjaro, imeamua kuanzisha utalii wa ndani ikiwa ni
jitihada za kumuunga mkono Waziri wa Maliasili na utalii, Dkt. Hamis
Kigwangala.
Kampuni hiyo
ya Rock-explorer imeanza jitihada hizo kwa ngazi ya chini ili kuweka uimara
zaidi katika sekta ya utalii, ambapo imeanza na kuhamasisha wanafunzi kupenda
kufanya utalii wa ndani.
“Tumeamua
kuanza na wanafunzi tukiamini kuwa wao watakuwa wajumbe wazuri katika jamii
yetu kwani watoto hawana sifa ya kupoteza kumbukumbu, hivyo watakuwa makini na
wenye mazoea ya kutembelea hifadhi za ndani na kuchangia pato la Taifa, alisema
George Mushi.”meneja wa kampuni hiyo.
Watoto
wamekuwa na uelewa wa hali ya juu na tunazidi kuwafundisha kwa vitendo ikiwemo
kutembelea hifadhi mbalimbali ili kukuza mabalozi wazuri pindi watakapo kuwa na
wengine.
Aidha
alisema familia nyingi za kitanzania hazina mazoea ya kutembelea hifadhi zetu
kama walivyo wenzetu wa mataifa mbalimbali na kuwaomba wazazi na wadau wengine
wawe na utaratibu wa kuwazoesha watoto kutembelea hifadhi za taifa kwani hazipo
kwa ajili ya wageni pekeyake.

No comments:
Post a Comment