Mkuu wa Operesheni maalum za Polisi, Naibu Kamishna wa
Polisi Liberatus Sabas akionyesha baadhi ya Silaha zilizokamatwa katika
Operesheni maalum ya kupambana na
uhalifu na wahalifu inayoendelea katika Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.
Wengine ni Maofisa mbalimbali waliopo katika Operesheni hiyo. (Picha na Jeshi
la Polisi).
Na. Jeshi la Polisi.
Jeshi la
Polisi nchini limefanikiwa kukamata Silaha mbalimbali na watuhumiwa 368 katika
Oparesheni Maalum inayoendelea katika Ukanda wa Kusini unaojumuisha mikoa ya
Lindi, Mtwara na Ruvuma.
Akizungumza mkoani Mtwara, Mkuu wa Operesheni Maalum za
Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema kati ya
watuhumiwa 368, 13 tayari wamefikishwa Mahakamani, 152 wamekabidhiwa
Idara ya Uhamiaji kwa hatua zaidi, tisa wapo chini ya Upelelezi na 194 wapo
chini ya uangalizi wa Polisi (Police Supervisee).
Sabas amezitaja
Silaha zilizokamatwa kuwa ni pamoja na SMG mbili, Pistol tano, Shotgun moja na
risasi 145, Visu 96, Makoti ya Sare za Jeshi la Msumbiji mawili, Raba za Jeshi la
Msumbiji jozi mbili pamoja na vifaa vya
kutengenezea milipuko.
“Baadhi
ya watuhumiwa ni wale waliokimbia katika Operesheni yetu ya Mkoa wa Kipolisi
Rufiji baada ya kuwazidi nguvu na sasa nawaambia tu wajisalimishe kwani hatuna
mchezo hata wakimbilie wapi mana tumepata taarifa kuwa wamejificha nchini
Msumbiji lakini kule napo wameanzisha operesheni kama hii“.
Alisema Sabas.
Aidha
Kamanda Sabas amesema Operesheni hiyo ni
endelevu na inashirikisha vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama hivyo ametoa
wito kwa raia wema kuendelea kutoa taarifa za siri ili kuendeleza amani na
usalama hapa nchini.
Hivi
karibuni Mkuu wa Jeshi la Polisi la nchini Msumbiji alikutana na IGP Simon
Sirro jijini Dar es Salaam kwa lengo kuboresha ushirikiano katika mapambano ya
uhalifu unaovuka mipaka ambayo ndio imekuwa changamoto katika nchi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment