Inaweza
kukuwia vigumu kuamini, lakini ndiyo hivyo tena, akiwa anatimiza umri wa miaka
68, miaka 39 ya kuwepo kwenye fani za michezo na burudani, hatimaye Mzee Juma
Mbizo ameamua kuingia studio kwa mara kwanza na kufanya ‘kolabo’ na mwanae
H-Mbizo.
Naam Mzee
Mbizo amejitosa katika studio za Fire Music chini producer More Fire na
kurekodi wimbo wa pamoja na H-Mbizo aliyepata kutamba na wimbo wa “Mchumba”.
H-Mbizo
ambaye pia mwandishi mzuri wa nyimbo akiwa amewaandikia wasanii wengi akiwemo
Snura kupitia wimbo “Majanga”, ameuambia mtandao huu kuwa kibao hicho
alichoimba na baba yake kitaachiwa hewani mwezi huu.
Licha ya
ukongwe wake kwenye game na utalaam wa kuandaa matamasha makubwa ya burudani,
lakini Mzee Mbizo hakuwahi kuingia studio na kurekodi wimbo wowote ule na hii
ndio hali itayofanya kazi hii alishoshirikishwa na mwanae iteke masikio ya
mashabiki wengi wa muziki.

No comments:
Post a Comment