Habari za Punde

TYSON FURY ALIVYOMCHAKAZA WILDER KWA TKO RAUNDI YA SABA


BONDIA Tyson Fury (kulia) amefanikiwa kumchakaza  mpinzani wake Deontay Wilder katika pambano la ngumi la marudiano la raundi 12 lililofanyika usiku wa kuamkia jana kwa TKO latika raundi ya saba.
Fury, anayefahamika kwa jina la 'The Gypsy King’ amekuwa Bingwa wa Masumbwi ya Uzito wa Juu wa Dunia wa WBC, na kuweka rekodi ya kuwa bondia namba moja kwa sasa kwenye uzito huo asiye na rekodi ya kupigwa kwenye mapambano yake yote, akiwa na sare moja ya pambano la kwanza dhidi ya Wilder.
Aidha, Fury ameweka rekodi ya aina yake kwa kuwa bondia wa kwanza kumchapa Wilder kwa kipigo cha TKO  ambaye mapambano yake yote ameshinda kwa KO isipokuwa pambano lao la kwanza mbalo lilimalizika kwa sare.
Katika pambano hilo  Fury,alimtesa Wilder akimpasua sikio lake na kusababisha damu nyingi kutoka huku watu wakisubiri mwamuzi tu amalize pambano.
Tangu raundi ya kwanza Fury alianza kwa kasi na kumpa presha kubwa Wilder ambayo ilimshinda kuhimili. Katika raundi ya 3, Fury alimpiga chini Wilder kwa mfululizo wa makonde mawili.
Fury ambaye ni bondia kutoka nchini Uingereza sasa ndiye mwenye nafasi ya kupambana na bondia mwenzake muingereza, Anthony Joshua.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.