Habari za Punde

TUWAPE FARAJA FAMILIA ZENYE WATOTO WENYE USONJI, TUSIWATENGE -JACKLINE MJEMA

 Mwandishi na Mtunzi wa Vitabu, Jackline Christopher akionesha kitabu chake cha All the Colors I See baada ya kukizindua mapema wiki hii ambapo kinazungumzia Mtoto mwenye tatizo la Usonji anayepitia changamoto baada ya kupoteza wazazi.

Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam.

Jamii  imetakiwa kutokuwatenga watoto wenye changamoto ya  Usonji ( AUTISM) na kuwapa faraja familia zenye watoto hao pindi wanapohitaji msaada mbalimbali.

Hayo yamesemwa na Mwandishi na Mtunzi wa Vitabu, Jackline Christopher Mjema wakati wa uzinduzi wa kitabu chake cha All the Colors I See kinachozungumzia mtoto mwenye changamoto ya  Usonji anayefiwa na wazazi wake na baadae ndugu kumpeleka kwenye kituo cha kulea watoto na huko ndipo anaingia kwenye maisha mengine mapya.

Jackline amesema, hiki ni kitabu chake cha tatu kuandika baada ya Hundred Sentences na Amnisia ambavyo vyote vinalenga kwenye masuala ya kijamii ikiwemk kitabu cha kwanza kinachozungumzia Maneno 'power of Sentence' , Amnisia ambavyo vyote aliviandika na vimefanya vizuri kwenye soko.

Amesema, amejikita zaidi katika masuala ya afya ya akili sababu jamii inahitaji kufahamu changamoto zilizopo ambapo awali alivyotunga kitabu cha Power Of Sentence ni kile kitu ambacho mtu anakifikiria ndani ya akili yake na baadae kwenda kukitenda na hiyo inakuwa ni nguvu ya maneno ndani ya akili ya binadamu.

"Hiki ni kitabu changu cha tatu, nimeweza kukiandika ni jambo la kumshukuru mungu na nilifikiria kuandika kitabu hiki baada ya kuona jamii bado haijawa na uelewa mkubwa juu ya masuala ya ugonjwa huu wa Usonji, jambo ambalo familia nyingi zimekuwa zinawatenga na kuona kama ni watoto au watu wasiokuwa na umuhimu," amesema Jackline.

Amesema, Kitabu hiki cha All the Colors I See kinaonesha ni namna ambavyo watoto wenye changamoto ya Usonji wanavyopata changamoto ya malezi pindi anapokosa upendo wa dhati kutoka kwa walezi wake baada ya Wazazi wake kufariki jambo ambalo linazidi kuwaathiri.Naye Moja ya wadau waliohudhuria kitabu hicho Bi. Ikupasifa ambaye ni mzazi wa mtoto mwenye Usonji amesema, alipitia changamoto kubwa sana kipindi anakuja kufahamu kama mtoto wake ana changamoto hiyo , ilifikia hatua ya kutaka kuchanganyikiwa.

Ikupasifa, watoto wenye Usonji wanahitaji sana upendo wa dhati kutoka kwa wazazi na anamshukuru aliweza kupata sapoti kubwa kutoka kwa mume wake katika kipindi chote ukitegemea baadhi ya wanawake wamekimbiwa na wenza wao baada ya kupata watoto wenye changamoto ya Ugonjwa wa Usonji.

Naye mdau na mwanahabari Zainabu Nyamka, ameshauri vyombo vya habari kuendelea elimu kwa jamii juu ya ugonjwa wa usonji kwani ili jamii itoke kwenye giza hili lazima uelewa uwepo. 

Ameshauri, vyombo vya habari kupitia mitandao ya kijamii, matukio makubwa mbalimbali ikiwemo makongamano watoe elimu sambamba na kuandaa vipindi vifupi vya mara kwa mara juu ya tatizo la Usonji ndani ya jamii yetu.

Kitabu hicho kimezinduliwa mapema wiki hii, kikigusa hisia za familia zenye watoto wenye usonji.



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.