Habari za Punde

*M-NET AFRIKA YAZINDUA MTANZAO WA 127 WA KURUSHA VIPINDI VYA KISWAHILI

Nembo ya M-Net Africa Magic Swahili.
Mkurugenzi Mtendaji wa M-Net Afrika, Biola Alabi, akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Africa Magic Swahili, ambao ni mtandao wa 127 uliozinduliwa kwa lengo la kuonyesha vipindi vya Kiswahili, MaigizoMuziki, Vichekesho pamoja na Filamu za Kiswahili, za Afrika Mashariki na Kati ambazo zitakuwa zikitafsiliwa kwa lugha ya Kingereza kupitia Dstv. Uzinduzi huo umefanyika leo mchana katika Hoteli ya Moven Pick jijini Dar es Salaam. Vipindi hivyo vinatarajia kuanza kuonyeshwa kuanzia tarehe 01, Mwezi Julai mwaka huu.Meneja Uhusiano wa Mult Choice Tanzania, Barbara Kambugi, akisaidia kurekebisha mitambo ili kuonyesha baadhi ya matangazo ya uzinduzi huo.
Pia baadhi ya wasanii walialikwa kuhudhulia uzinduzi huo, pichani ni Mama yake Monalisa, Natasha akipozi na msanii mwenzake, Deogratius Shija, wakati wa uzinduzi huo.
Steven Kanumba, pia alikuwa ni miongoni mwa wasanii waliohudhulia uzinduzi huo.
Msanii Deogratius Shija na wenzake wakiwa ukumbini humo, kuhudhulia uzinduzi huo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mult-Choice Tanzania, wakiwa ukumbini kuhudhulia uzinduzi huo.
Monalisa na Mama yake Natasha, wakipozi pamoja kuhudhulia uzinduzi huo.
Ray, Cloud na Chopa, wakifuatilia uzinduzi huo.
Na wadau pia walialikwa katika uzinduzi huo, Sufianimafoto (kulia), Amour Hassan Mhariri wa gazeti la Nipashe upande wa Michezo na Shamim Mwasha, mmiliki wa mtandao wa 8020 Fashion, wakihudhulia uzinduzi huo.
Hili lilikuwa ni pozi la uchokozi la wanabloger, Sufianimafoto na 8020fashion.
Kutoka (kushoto) ni Boniface Makene, Jennifer Sumi wa Mo Blog, Zainul Mzige wa Mo Blog, mmiliki wa mtandao huu, Sufianimafoto, Shamim Mwasha wa 8020 Fashion na Mzee wa fullshangwe, wakipozi kwa picha.




No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.