Habari za Punde

*KAGAME CUP-YANGA YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA NA EL-MEREIKH

 Mashabiki wa timu ya Yanga ya Dar es Salaam, wakishangilia jukwaani baada ya Yanga kuandika bao la pili katika kipindi cha kwanza, lililofungwa na Asamoh, baada ya krosi safi kutoka kwa Kigi Makasi, na kufanya timu hizo kwenda mapumziko Yanga ikiwa mbele kwa mabao 2-1. Kipindi cha pili Wasudani waliweza kupata bao lililozua utata baada ya kugonga mwamba wa juu na kisha kurudi uwanjani na kudakwa na mlinda mlango wa Yanga, huku Mwamuzi wa mchezo huo akiashiria kuendelea kwa mchezo ambaye alitofautiana na mshika kibendera wake aliyeonysha kuwa ni goli na kumfanya mwamuzi kuwa na maamuzi mawili, huku akinyoosha mikono kuashiria kuendelea kwa kipute na wakati huo huo akipuliza kipenga cha kuonyesha kati kuashiria goli.
 Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Godfrey Bony, akiwa jukwaani na mashabiki wa Yanga akifuatilia kipute hicho, kutokana na kutokuwa kabisha katika risti ya Timbe.
 Raha ya mechi Bao bwana!!!, hapa ni Mhariri wa Gazeti la Champion, Elius Kambili,  ambaye pia ni shabiki wa Yanga, akishangilia na kuonyesha alama ya 2, baada ya Yanga kufunga bao la pili.
 Mashabiki wa Soka wakikata tiketi na kupanga foleni ili kuingia ndani ya uwanja kushuhudia kipute hicho. Katika mchezo wa leo watu walikuwa wengi tofauti na jana kiasi kwamba wengine walikosa tiketi walizokusudia kununua baada ya tiketi ya Sh. 2000 kuuzwa kwa Sh. 6000 na nyinginezo kupandishwa bei baada tu ya mpira kuanza.
Kipute kinaendelea uwanjani.......ilikuwa ni kipindi cha kwanza.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.