Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL MGENI RASMI KILELE CHA SIKU YA MADAWA YA KULEVYA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Tatu Mapando, ambaye ni mmoja kati ya vijana waliotoa ushuhuda mbele ya Makamu wa Rais kuhusu matumizi ya madawa ya kulevya, baada ya kuacha kutumia madawa hayo. Tatu aliwahi kuwa mnenguaji wa muziki wa dansi katika bendi za Fm, Academia, Diamond Sound, Betta Musica na bendi kadhaa za jijini kabla ya kuanza kutumia madawa.
Muelimisha Rika kutoka Banda la Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya, Catherine Saoke, akifafanulia jambo wanafunzi wa Shule ya Msingi, Kilimahewa ya Temeke, Mubaraka Abdallah na Ally Kionda, kuhusu utofauti na madhara kati ya dawa ya Cocaine na Heroin, wakati wanafunzi hao walipotembelea Banda hilo kwenye Kilele cha Maadhimisho ya    Siku ya Kupiga vita Biashara na Matumizi ya Madawa ya Kulevya, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya madawa ya kulevya yaliyokuwa katika moja ya mabanda hayo kwa ajili ya maonyesho.
Vijana waliokuwa wakitumia madawa ya kulevya, Rajab Huseein na Tatu Mapando, wakitoa ushuhuda kuhusu utumiaji wa madawa ya kulevya baada ya kuacha kutumia madawa hayo.
"Hapa ujumbe utafika kwa wajukuu". Bibi Kizee akipita mbele ya mabanda kukusanya vipeperushi katika kilelel cha maadhimisho ya siku ya kupiga vita madawa ya kulevya.
Wanafunzi kutoka Shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam, wakipita mbele ya jukwaa la mgeni ramsi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na mabango yenye ujumbe mbalimbali kuhusu suala zima la kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya.
Wanafunzi kutoka Shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam, wakipita mbele ya jukwaa la mgeni ramsi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na mabango yenye ujumbe mbalimbali kuhusu suala zima la kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya.
"BABA TUMEKOMA BABA KUTUMIA MADAWA" Baadhi ya vijana waliowahi kutumia madawa ya kulevya wakipita na mabango mbele ya jukwaa la mgeni ramsi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, yenye ujumbe wakitaka kusaidia dawa na Serikali dawa za kuzuia kutumia madawa, wakati wa Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kupiga vita Biashara na Matumizi ya Madawa ya Kulevya.
Kikundi cha Sanaa cha Temeke, kikitoa burudani wakati wa sherehe hizo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Rashid Abdallah wa IOGT  wakati alipotembelea na kukagua mabanda katika Viwanja vya Mwembe Yanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkemia Mkuu wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Bertha Mamuya (katikati) wakati alipotembelea na kukagua mabanda katika Viwanja vya Mwembe Yanga.
Baadhi ya Vijana wakiingia kwenye viwanja hivyo kwa maandamano ya staili ya kufanya mazoezi na kuimba.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.