Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbezi Mtoni jijini Dar es Salaam, eneo la Mbezi juu, Joseph, amedaiwa kuanza kutangaza biashara ya kuuza nyumba yake.
Jose, amefikia hatua hiyo baada ya kashfa za hivi karibuni zilizomkuba za kuuza viwanja vya wananchi na kubomoa nyumba za wananchi kiasi cha kuchukuliwa hatua na kukamatwa na polisi na kisha kutupwa lupango.
Aidha imeelezwa kuwa kutoka na tayari alikwishauza viwanja hivyo kwa watu na kupokea pesa na baadaye dili hilo likaingia dosari baada ya wananchi kushtukia na kuvamia maeneo hayo na kuanza kujenga, tayari Jose anamaedi kadhaa ya mamilioni ya fedha anazodaiwa na aliowauzia viwanja baada ya kushindwa kuwapatia viwanja hivyo na kesi ipo Polisi.
Aidha imeelezwa kuwa Jose alifanya maamuzi ya kuisafirisha familia yake na kuanza kutangaza kuuza nyumba yake ili aweze kupata fedha za kuandaa kundi la kufanya vurugu na kubomoa nyumba za wananchi zilizojengwa katika maeneo hayo aliyotaka kuuza viwanja na kisha atimke zake kusikojulikana.
Imeelezwa kuwa zoezi hilo lilinyimwa baraka zote na wanafamilia yake na kumueleza kuwa endapo atafanya hivyo basi hawatakuwa naye bali watakuwa upande wa pili na kumfichua kokote atakakojificha, jambo lililomfanya kuirejesha tena familia yake nyumbani na kuanza kupanga ,mbinu mpya.
Asiye kubali kushindwa si mshindani!, naam huo ni usemi wenye maana zaidi kwa mtu anayeongozawatu na mwenye busara zake, Wananchi waliojenga maeneo hayo hawakujiamulia bali ni baada ya kuona haki yao inapotea tena kwa mtu mmoja mmoja binafsi tena kwa kuwapa watu wasiokuwa wazawa wa eneo hilo, na ndipo wakaona njia rahisi ya kulinda eneo hilo basi ni kuvamia na kujigawia maeneo na kisha kuanza kujenga.
Nani wa kulaumiwa Wananchi walioamua kulinda eneo lao kwa njia ya kuendeleza makazi, ama Mwenyekiti aliyekuwa akiwapiga changa la macho wananchi kuwa ni eneo la maendeleo hali ya kuwa akimega vipande kinyemela na kuuza?????? Na kuuza nyumba ili kupambana na wananchi hiyo ni akili au matope??

No comments:
Post a Comment