Rais Chiluba aliiongoza Zambia kwa mwongo mzima katika miaka ya '90, na baada ya kustaafu alishtakiwa kwa kutuhumiwa na rushwa.
Frederick Chiluba, alianza kuiongoza Zambia mwaka wa 1991, wakati Afrika ikianza kuingia katika mikakati ya demokrasi ya vyama vingi, ambapo awali aliwahi kuwa kiongozi wa wafanyakazi.
Wakati akiingia madarakani aliahidi kuleta mabadiliko makubwa ya maendeleo , lakini mara tu ya kuchukua uongozi tayari Zambia ilikuwa imeshafilisika, naye alishindwa kuchukua hatua ya kuzuia rushwa na kuiacha ilizidi kustawi.
Alipojaribu kujiongezea muhula wa tatu wa madaraka, alipingwa ‘Piya’ akilaumiwa kuwa akipenda maisha ya anasa na kuiacha nchi ikizidi kuangamia kiuchumi.
Baada ya kuondoka madarakani mwaka wa 2001, mrithi wake, Levy Mwanawasa, alimshtaki kwa kosa la kuwa mla rushwa.
Baada ya kesi ya miaka 6 kuhusu ubadhirifu wa mali ya Umma wa Taifa hilo, Chiluba, alishinda kesi hiyo na kuambiwa kuwa hakupatikana na makosa.
Lakini katika kesi nyengine iliyoendeshwa katika Mahakama Kuu ya London, Chiluba, alipakana na hatia ya kuiba mamilioni ya dola ya fedha za serikali ya Zambia, kwa kutumia akaunti za kwenye mabenki ya London.
No comments:
Post a Comment