Wanafunzi wa kike katika shule ya msingi Manda wilaya ya Ludewa ambao wanasubiri kufanya mtihani wa Taifa wa Darasa la saba wakitoka kuokota kuni porini mida ya masomo baada ya kufukuzwa kwa kushindwa kulipa mchango wa shilingi 600 ili wapate kufanya mitihani ya kujipima ya kata mzigo wa kuni kama huu wamekuwa wakiuuza kwa kiasi cha shilingi 100 kwa walimu wao.
WAZAZI wa wanafunzi wa darasa la saba ambao wanangoja mtihani wa Taifa wa kuhitimu elimu ya msingi katika shule ya msingi Manda wamekuwa na hofu ya watoto wao kufeli mtihani wa Taifa wa darasa la saba kutokana na uongozi wa shule hiyo kuwafukuza wanafunzi wasio kulipa mchango wa shilingi 600 michango ya mitihani na wakati mwingine kuwatuma kutafuta kuni za walimu.
Wakizungumza na mtandao huu wazazi hao JOhn Haule na Hosea Nkera walisema kuwa tabia ya uongozi wa shule hiyo kuwafukuza madarasa ni wanafunzi hao wa darasa la saba wasio lipa mchango wa shilingi 600 iwapo haita kemewa upo uwezekano wa watoto wao kufanya vibaya mtihani huo.
Kwani walisema kuwa wakati shule nyingine za msingi kwa wakati huu wa kuelekea katika mtihani wa Taifa wa darasa la saba walimu wamekuwa wakikesha wakiwakumbusha watoto yale waliyofundishwa ili kujiweka vizuri kwa mitihani hiyo ila shule hiyo imekuwa ikitumia muda mwingi kuwatumikisha wanafunzi hao katika kazi za
walimu za kutafuta kuni porini na kufanya kazi nyingine za walimu huku baadhi yao wakifukuzwa kufuata michango kwa wazazi.
Alisema Haule kuwa baadhi ya wazazi katika kata hiyo ya Manda wana hali mbaya kiuchumi na hawana fedha za kuwalipia wanafunzi hao kiasi hicho cha shilingi 600 kwa ajili ya kufanya mtihani wa kujipima na kupelekea idadi kubwa ya wanafunzi hao wa darasa la saba kujiingiza katika shughuli za uvuvi katika ziwa nyasa kutafuta samaki wa kuuza ili kupata fedha hizo na wale wasio na uwezo wamekuwa wakilazimika kushinda mitaani .
Hivyo alimwomba afisa elimu wa wilaya hiyo ya Ludewa na serikali kupiga marufuku walimu kuwatumikisha ama kuwafukuza wanafunzi hao wa darasa la saba wasio na michango kwani kufanya hivyo ni kupelekea matokeo ya ufaulu kwa wanafunzi hao kuwa mabaya zaidi.
Huku Nkwera akitaka walimu kutowasumbua wanafunzi hao kwa michango na kuwa iwapo shule kunamradi unaendeshwa basi uwe kati ya wazazi na wananchi wote wanaozunguka shule husika badala ya kuwalenga wanafunzi pekee ambao hawana uwezo wa kupata fedha hizo.
Alisema kwa upande wake ana watoto wawili ambao wanasoma shule hiyo darasa la saba na kuwa uwezo wa kuwalipia shilingi 1200 kwa ajili ya mtihani kwa sasa hana .
Mmoja kati ya walimu wa shule hiyo ambaye hakupenda kutaja jina lake kwa madai kuwa si msemaji wa shule hiyo alisema kuwa utaratibu huo wa michango uliamuliuwa katika kikao cha pamoja kati ya wazazi na viongozi wote wa kata hiyo ya manda na kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya kuchangia gharama za usimamizi wa mitihani na chakula kwa walimu wanaofika kusimamia mitihani ya kujipima ngazi ya kata.
Diwani wa kata ya Manda Efrida Kizota alisema kuwa hakuna kikao ambacho kilikaa na kuamua wanafunzi kuchangia gharama za mkitihani na kuwa uongozi wa shule hiyo unafaya makosa kuwafukuza wanafunzi kwa kufuata michango hiyo isiyo na baraka kutoka kwa wazazi na wananchi.
Afisa elimu wa shule za msingi wilaya ya Ludewa Robart Hyella alisema kuwa amepokea malalamiko ya wazazi juu ya walimu wa shule hiyo kufukuza wanafunzi kwa ajili ya kukosa michango na kuwa amemwagiza mratibu wa elimu kata kufuatilia suala hilo.
No comments:
Post a Comment