Habari za Punde

*KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO


Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema, akitoa ufafanuzi kuhusu masuala  mbalimbali ikiwemo hotuba iliyotolewa jana na Godbless Lema  ambaye ni msemaji  mkuu wa kambi ya upinzani kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya wizara Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2011/2012. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) William Lukuvi. Picha Zote na Anna Nkinda-MAELEZO
Mbunge wa Bumbuli  (CCM) January Makamba  akimuuliza swali waziri wa Nishati na Madini kuwa Serikali inampango gani wa kuendeleza  mradi wa umeme katika kata ya Mgwashi leo  katika kipindi cha maswali na majibu kwenye Mkutano wa nne wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli (katikati) akifurahia jambo na  Mbunge wa Vunjo (TLP) Augustino Mrema(kushoto) na Mchungaji Israel Natse (CHADEMA)  (kulia) Mbunge wa Karatu kabla ya kuanza kwa  kikao cha thelathini  na sita katika mkutano wa nne wa bunge unaoendelea  mjini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Shamsi Vuai Nahodha (kushoto) na Naibu waziri wake Balozi Khamis Kagasheki, wakiandika michango mbalimbali iliyokuwa inatolewa na wabunge kuhusu bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo leo kwa mwaka wa fedha 2011/2012 Bungeni leo mjini Dodoma.
Mbunge wa Maswa Mashariki (CHADEMA) Sylvester Kasulumbai, akichangia   hoja kuhusu bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2011/2012 Bungeni leo mjini Dodoma.
 Mbunge wa Mtera (CCM) Livingstone Lusinde akitoa mwongozo kwa Mwenyekiti wa Bunge  Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa kikao cha thelathini na tano kilichofanyika jana mjini Dodoma kuwa wabunge wote wakapimwe akili hii ni kutokana na matukio ya uvunjifu wa kanuni yanayotokea mara kwa mara ndani ya Bunge.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.