Zile Sarakasi na mambo ya Utoto yameendelea tena jana Mjengoni baada ya juzi, Mbunge mmoja kutolewa nje kwa kutofuata taratibu za uendeshwaji wa shughuli za Mjengoni, ambapo Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai, aliyekuwa akiongoza kikao cha jana kabla ya kuanza shughuli hiyo alianza kwa kuwaonya waheshimiwa Wabunge na kuwakumbusha muongozo na taratibu za uendeshwaji wa vikao vya Bunge.
Baada ya hapo alifungua rasmi kikao, lakini wakati kikao hicho kikiendelea kama ilivyo ada waheshimiwa walianza 'kuintafia' mazungumzo aliyokuwa akiyawakilisha Mbunge Tundu Lissu huku wengine wakiwasha 'Mic' na kuchombeza maneno na wengine wakishangilia kwa staili ya kugonga meza kulikopitiliza, jambo ambalo lilimshinda kuvumilia Naibu Spika, Job Ndugai na kuamua kuwatoa nje waheshimiwa watatu, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, Mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema. Na hatimayeleo katika magazeti yote yameendelea kutoka na Comedy hiyo.
No comments:
Post a Comment