Habari za Punde

*LADY JAY DEE KULA DINNER NA WACHEZAJI WA YANGA LEO NYUMBANI LOUNGE


Na Mwandishi Wetu, jijini Dar
MWANAMUZIKI Nyota wa kike nchini Lady Jay Dee akishirikiana na  Uongozi wa Klabu ya Yanga kwa pamoja wameandaa tafrija fupi ya chakula cha jioni kwa lengo la kuwapongeza wacheazaji kwa ushindi wa kutwaa kombe la Kagame katika michuano iliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kuwaadhibu Watani wao wa Jadi Simba.

Ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha furaha ya ushindi wa  kutwaa Kombe hilo  inaendelea, wachezaji hao watakutana katika Mgahawa wa Nyumbani Lounge leo jioni ili kula Bata kwa pamoja huku wakisebeneka na miondoko ya muziki wa Binti Machozi. 

Aidha uongozi wa maandalizi ya tafrija hiyo umesema kuwa pamoja na tafrija hiyo lakini pia wadau wa Klabu hiyo wamejitokeza na kuichangia timu yao kiasi cha Sh. milioni 40, na kuongeza kuwa tafrija hiyo ni maalum kwa ajili ya kuwapongeza wachezaji kwa ushindi huo na si vinginevyo.

Mbali ya wadau hao waliokunwa na ushindi huo kuchanga fedha hizo, pia uongozi utawaongezea ‘wapiganaji’ hao kwa asilimia 80 ya mapato yaliyopatikana katika mechi ya fainali iliyopigwa Jumapili iliyopita Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Naye Katibu Mkuu wa Klabu hiyo Mwesigwa Celestine, alisema kuwa baada ya mchezo huo wachezaji wote walikuwa katika mapumziko mafupi na wanatarajiwa kurejea kambini Julai 20.

Aidha alisema ushindi walioupata ni uthibitisho tosha kwamba wanaweza, japokuwa walifungiwa miaka mitatu na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Akizungumzia kuhusu motisha hio, alisema wadau mbalimbali wa soka nchini wamewazawadia wachezaji jumla ya sh milioni 40 na wao kama uongozi umepanga kuwapa asilimia 80 ya mgawo wao watakaopata katika mechi ya fainali.

Pia katika hatua nyingine, Mwesigwa alikanusha taarifa zilizotolewa kuwa, beki wao, Nadir Haroub ‘Canavaro’, amechukuliwa na El Mereikh ya Sudan.

Mwesigwa alisema, anashangazwa na taarifa hizo na kwamba hazina ukweli, kutokana na wao kutopata tamko lolote kutoka kwa El Merreikh.
Habari hii kwa hisani ya Blog ya Dina Ismail

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.