Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akiweka Ngao, katika Mnara wa Mashujaa mahala walipozikwa Mashujaa 101 waliopigana vita Msumbiji, ikiwa ni siku ya sherehe ya kuwakumbuka Mashujaa iliyofanyika kwenye Viwanja hivyo vilivyopo Naliendele mkoani Mtwara leo.
Balozi wa Congo DRC, ambaye pia ni kwa niaba ya Mabalozi waliohudhuria maadhimisho hayo, Juma Alfan Mpango, akiweka shada la maua kwa niaba ya malozi.
Meya wa Mtwara-Mikindani, Seleman Mtalika Shiringi, akiweka Rungu na Upinde katika Mnara wa Mashujaa.
Askari, wakipiga Wimbo wa Taifa.
Sehemu ya Makaburi ya Mashujaa hao 101 kati ya 108, waliohamishwa mwaka 2004 kutoka Msubiji walikokuwa wamezikwa baada ya kufariki katika vita, ambapo walikuwa ni miongoni mwa askari waliokuwa wakisaidia kupatikana kwa amani nchini Msumbiji baada ya kuwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Mnara wenye majina ya Mashujaa hao.
Askari wakitoa heshima katika Mnara huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete na Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakitembelea kukagua makaburi 101 kati ya 108, ya askari ‘Mashujaa’ walifariki wakati wakipigana vita Msumbiji na kuzikwa katika Makaburi ya Naliendele mkoani Mtwara, wakati wa sherehe za kumbukumbu za Mashujaa zilizofanyika leo, mkoani Mtwara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wake wa pili, Balozi Seif Ali Idd, wakitembelea na kukagua makaburi ya Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Mashujaa iliyoadhimishwa katika viwanja vya makaburi ya Mashujaa Naliendele, mkoani Mtwara le.
Rais Jakaya Kikwete, akiwahutubia wananchi wakati wa maadhimisho ya siku ya Mashujaa, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Makaburi ya naliendele mkoani Mtwara.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya sherehe hizo.
Viongozi wa Dini wakiomba dua wakati wa maadhimisho hayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimia wananchi katika sherehe hizo.
Baadhi ya askari wazee wastaafu waliopigana vita.
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakitembelea Chumba cha Makumbusho cha Mashujaa kilichopo katika Viwanja hivyo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Wazee waliopigava Vita, ambao ni sehemu ya mashujaa wa Tanzania, wakati wa maadhimisho ya Siku ya mashujaa iliyofanyika kwenye viwanja vya naliendele, Mkoani Mtwara leo
No comments:
Post a Comment