Hii sasa inazidi kukera masikioni na machoni mwa wananchi na hasa wanaoamini kuwa wamewatuma wawakilishi imara katika kuwawakilishia matatizo yao Bungeni, na pindi wanapowaona katika picha za magazeti kama hivi ama katika Tv na kuwasikia katika redio kwa kweli inakera.
Siku za nyuma Vijana walikuwa wakilalama kuwa wanatengwa kwa kutopewa fulsa ya kuingia Mjengoni kuonyesha na kuchangia mawazo yao mapya yanayoendana na mabadiliko ya Dunia huku wakiwabeza wazee eti kuwa wanalala Mjengoni na kushindwa kuchangia vikao vya Bunge huku wakitazamwa na wananchi wao, jambo ambalo liliwaamsha vijana wengi kwa kipindi hiki wakitaka kuwania nafasi za Ubunge ili kuwawakilisha wananchi wao ipasavyo.
Lakini vijana hao hao waliotazamiwa kuleta changamoto na mabadiliko ndani ya bunge ili kuonekana ni bunge la kisasa zaidi ndiyo hao hao wanaoleta "Utoto Mjengoni" Mambo kama haya hayakuwahi kutokea kamwe siku za nyuma tena katika Mahala muhimu kama Bungeni na panapostahili heshima ya pekee kiasi cha wabunge kufikia kutaka kutiana vidole vya macho huku wakisutana kana kama watoto huku wengine wakileta utani wa kishule shule wakigushi saini ya waziri Mkuu. "Hii Imezidi inabidi hatua ya kusemea na kukemea tabia hii itolewe ili kuzuia isizidi kukua na kutufikisha tusipopataka watanzania" Haya ni Mawazo yangu Wadau.
No comments:
Post a Comment