Gire akiwa na uso wa furaha wakati akitoka kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kuachiwa huru leo. |
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dar es Salaam, imemwachia huru, Naeem Gire, aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya kughushi na kuidanganya Serikali kuwa mitambo ya kuzalisha umeme ya ‘Richmond’ ina uwezo wa kufua megawati 100 za umeme.
Baada ya kuachiwa huru mshitakiwa huyo, Gire, alitoka kizimbani akichekelea baada ya hakimu wa mahakama hiyo, Waliarwande Lema , kutamka kuwa anamuona mshitakiwa huyo kuwa hana kesi ya kujibu kutokana na ushahidi uliotolewa na upande wa Serikali uliofikishwa mahakamani hapo kushindwa kukidhi vigezo vya kumtia hatiani.
“Baada ya kupitia ushahidi katika vipengele vyote, nimeona kuwa hakuna ushahidi wa kutosha uliowasilishwa ukionyesha kuwa mshitakiwa ana hatia na kuwa na kesi ya kujibu,

Kesi hii ni miongoni mwa kesi kadhaa ambazo huletwa mahakamani na kisha kuitwisha lawama mahakama", alisema Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Waliarwande Lema.
No comments:
Post a Comment