Habari za Punde

*USIKU WA KOPO KURINDIMA JIJINI DAR


Kampuni ya Entertainment Masters Limited magwiji wa burudani nchini, wameamua kuja kivingine na kutoa burudani ya aina yake.
Usiku huu maalum ujulikanao kama usiku wa Kopo itatawaliwa na nderemo, muziki na vinywaji mbali mbali vya kopo. Lengo haswa ni kuwapa burudani wakaazi wa Temeke na vitongoji vyake.
Usiku wa Kopo katika wilaya ya Temeke itafanyika Ijumaa tarehe 22 Julai 2011 katika Viwanja vya TCC Sigara Chang’ombe.
Burudani ya muziki wa kizazi kipya itatolewa na CPWAA,Joh Makini, Mr.Blue, Belle 9, Gangwe Mob, Daz Baba, 20 per cent na Sir Juma Nature.
Lengo la USIKU WA KOPO ni kutoa burudani yenye hadhi ya kimataifa kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam na inayopatikana kupitia kituo cha runinga ya DTV.
USIKU WA KOPO ina lengo la kutoa asante kwa wakazi wa Dar es Salaam kwa kuichagua DTV kama kituo chao bora cha runinga.
Pia Usiku wa Kopo itawakutanisha wanafunzi wa vyuo na kuwapa fursa ya kubadilishana mawazo.
Muziki katika Usiku wa Kopo itaporomoshwa na MaDJ toka Club Maisha ya jijini Dar es Salaam. Madj hao mahiri ni DJ Zero na DJ Tariq.
Mbali na muziki wa kizazi kipya, kutakuwepo na burudani mbalimbali pia kutakuwepo na zawadi kutoka kwa wadhamini.

Penniel Mungilwa
Meneja Uhusiano

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.