Habari za Punde

*VODACOM YADHAMINI MAONESHO YA NANENANE 2011 DODOMA

 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhandisi Pius Msekela (Wa pili Kulia) akiangalia ubora wa simu 20, Tshirt 300 na fedha taslimu shilingi milioni 15/- alizopokea kutoka kwa Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania Kanda ya kati, Macfaydyne Minja, zitakazotumika kwa ajili ya mawasiliano na maandalizi ya Maonesho ya Nanenane mwaka huu. Katikati ni Atilia Lupala ambaye ni Mkuu wa kanda ya Pwani wa kampuni hiyo (kulia) ni Dkt. Samson Muniko Katibu wa Taso kanda ya kati . Picha kwa Hisani ya Vodacom.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhandisi Pius Msekela ( Kulia) akimsikiliza Mtaalam wa Masuala ya Habari wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (Wa pili kushoto) wakati wa hafla ya makabidhiano wa simu 20, Tshirt 300 na fedha taslimu shilingi milioni 15/- zitakazotumika kwa ajili ya mawasiliano na maandalizi ya Maonesho ya Nanenane mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhandisi Pius Msekela ( Kulia) akiteta jambo na Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania (Kutoka kushoto) na Meneja Mauzo kanda ya kati Macfaydyne Minja, Atilia Lupala ambaye ni Mkuu wa kanda ya Pwani na Mtaalam wa Masuala ya Habari wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.