Habari za Punde

*YALIYOJIRI BUNGENI DODOMA LEO, WENJE ATOLEWA NJE, WABUNGE WASUTANA NJE YA BUNGE NUSURA KUCHOMANA VIDOLE VYA MACHO

 Mbunge wa Nyamagana (CHADEMA)  Ezekia Wenje (aliyevaa suti ya rangi ya maziwa) akitolewa nje ya ukumbi wa Bunge na  Askari Polisi wa Bunge baada ya kutomtii Mwenyekiti wa kikao  cha Bunge cha leo Mbunge wa Dole (CCM) Silvester Mabumba, alimtaka kukaa chini na kutokutoa hoja ya dharula kuhusu Samaki wa sumu kutoka Japan. Picha Zote na Anna Nkinda-MAELEZO

 Mbunge wa Nyamagana (CHADEMA)  Ezekia Wenje (aliyevaa suti ya rangi ya maziwa) akitolewa nje ya ukumbi wa Bunge na  Askari Polisi wa Bunge.

Baadhi ya mawaziri wakimpongea waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Prof. Jummanne Maghembe mara baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya wizara yake  jana jioni katika kikao cha Bunge la bajeti kinachoendelea mjini Dodoma.

NJE YA UKUMBI WA BUNGE


 Mbunge wa Ludewa  (CCM) Deo Filikunjombe (kushoto)  akisutwa nje ya ukumbi wa Bunge na Mbunge wa viti Maalum (CHADEMA) Suzan Kiwanga (aliyevaa kitenge) baada ya  Filikunjombe kumwambia, Ezekia Wenje, mbunge wa Nyamagana (CHADEMA) (hayupo pichani) alikosa  ustaarabu kwa kutokumtii Mwenyekiti wa kikao  cha Bunge cha leo Mbunge wa Dole (CCM) Silvester Mabumba pale alipomwambia akae chini na kutokutoa hoja ya dharula kuhusu Samaki wa sumu kutoka Japan.

 Mbunge wa Ludewa  (CCM) Deo Filikunjombe (kulia)  akisutwa nje ya ukumbi wa Bunge  na wabunge wa viti Maalum (CHADEMA) Philipa Mturano (kushoto) Suzan Kiwanga  (aliyevaa kitenge) na  Mbunge wa jimbo la Kasulu mjini (NCCR – MAGEUZI) Moses Machari.

 Mbunge wa Ludewa  (CCM) Deo Filikunjombe (kushoto)  akisutwa nje ya ukumbi wa Bunge  na baadhi ya wabunge wa upinzani Moses Machari (kulia),  Philipa Mturano (katikati) na Ezekia Wenje (kushoto) baada ya  Filikunjombe kumwambia Wenje kuwa  alikosa  ustaarabu kwa kutokumtii Mwenyekiti wa kikao  cha Bunge cha leo Mbunge wa Dole (CCM) Silvester Mabumba pale alipomwambia akae chini na kutokutoa hoja ya dharula kuhusu samaki wa sumu kutoka Japan.

Mbunge wa Ludewa  (CCM) Deo Filikunjombe (kulia)  akisutwa nje ya ukumbi wa Bunge  na wabunge wa viti maalum (CHADEMA) Philipa Mturano (kushoto ) na Maryam Msabaha (katikati). 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.