Habari za Punde

*YALIYOJIRI MECHI YA WATANI WA JADI YANGA NA SIMBA KAGAME CUP JANA

 Mashabiki wa Yanga, wakishangilia huku wakiwa na mdoli ulioandikwa jina la kipa wa Simba Juma Kaseja, wakiwa wamemvisha Shanga. Mashabiki hao hawakumuonyesha mdoli huyo kabla na wakati mpira ukiendelea bali baada ya kufungwa goli tu walimuibua juu na kuanza kumrusharusha huku wakipiga kelele kumuonyesha mdoli wao huyo......."Huu ndiyo mtanange wa Watani wa Jadi."
 Mashabiki hao hao wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali wa kuwakebehi Simba na picha ya Salun inayomuonyesha mdada ambayo wameiandika jina la Kipa wa Simba Juma Kaseja. .... "Sijui hii inamaanisha nini".
 Mashabiki wa Simba wakiwa tuliiiivu, wakati mtanange huo ukiendelea....."Sijui walihisi nini".
 Ni vijembe na utani tu ukiendelea katika Jukwaa la Yanga wakiwakebehi Watani zao Simba..."Hii no Comment".
 Ilikuwa ni shangwe Furaha na nderemo baada ya kufungwa kwa goli lisilo na utata la ushindi, lililofungwa na Asamoh, muda mchache tu baada ya kuingia akitokea Benchi....."Hii ilikuwa ni siku ya Wanajangwani".
 David Mwape wa Yanga (kulia) akichuana na beki wa Simba Kelvin Yondan, wakati wa mtanange huo.
 "Hapa Hupiti wewe bwana mdogo", Ndivyo anaonyesha kukamia na kusema Amir Maftah wa Simba (kulia) wakati akimdhibiti winga wa Yanga, Godfrey Taita.
 Askari wakimuondoa eneo la Simba, mpigapicha wa gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga, (katikati) aliyekuwa ametinga T-Shirt ya njano huku akiendelea kuchapa mzigo akiwa nyuma ya goli ya Simba kama ilivyoa ada ya wapiga picha kuchagua goli alipendalo ili kupata 'Shoti anayoihitaji' ama anakoona kuna mashambulizi ya kila mara. Mashabiki wa imba walianza kurusha mawe, chupa za maji huku wakipiga makerere wakimtaka kuondoka eneo hilo kwa kile walichodai rangi ya nguo aliyovaa haiendani na eneo alilokaa. Baada ya hapo nao Mashabiki wa Yanga walianza mashambulizi wakiwarushia vyupa na mawe na makerere lukuki wakiwataka wafanyakazi wa Huduma ya Kwanza Red Cross kuondoka mbele ya jukwaa la Yanga eti nao kwa vile wametinga nguo zenye alama nyekundu na nyeupe zinazoashiria Simba, haraka sana nao waliondolewa na askari na baada ya kurejea uwanjani waliamua kuketi sehemu moja tu mbele ya Jukwaa la Simba, hapo ngoma ikawa droo..... "Hivi ni sehemu tu ya vijimambo vilivyotokea uwanjani hapo".
 Godfrey Taita, akichuana na Amir Maftah...
 Mshambuliaji wa Yanga, Hamis Kiiza wa(kulia) akimtoka beki wa Simba, Nasoro Chollo, wakati wa mtanange huo. 
 Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Nurdin Bakar, akichuana na Kelvin Yondan.
 Kipa wa Simba Juma Kaseja, akiruka kudaka mpira mbele ya Keneth Asamoh wa Yanga.
 Hili ndilo goli lililofungwa na Keneth Asamoh kwa shuti kali la kichwa, na kumuacha kipa wa Simba Juma Kaseja, akichumpa kujaribu kuokoa mpira huo bila mafanikio. La! la! la! goooooooo!
 Hamis Kiiza akiruka kumpongeza Keneth Asamoh, baada ya kufunga goli hilo......
 Rashid Gombo ni kama 'Balotelli', Julius Mlope (kushoto) na Nurdin Bakar, wakimpongeza Rashid Gumbo baada ya krosi nzuri iliyozaa bao la ushindi, lakini Gumbo yeye kama hayupo kabisa hukua kiwa kakunja uso akiwakazia macho Benchi la Simba.....
 Ilikuwa ni furaha kwenda mbele baada ya kumalizika kwa mtanange huo, hapa ni wachezaji wa Yanga wakishangilia huku wakikimbia uwanja mzima  huku wakipeperusha bendera....
 "Raha ya Mechi Baooooo, Haya weee haya weee"......
 Kipa wa Yanga Yaw Berko (kulia) na mshambuliaji Keneth Asamoh, wakiomba Mungu baada ya kumalizika kwa mchezo huo, "Hawa ni miongoni mwa wchezaji waliofanya vizuri katika safu ya Yanga jana"
 Makipa wa Yanga, wakipongezana.......... 
 Utani unaendelea "sijui walikuwa wakimaanisha nini".........
 Ridhiwani Kikwete na swahiba wake Mudy Sebene, wakishangilia ushindi wa Yanga uwanjani hapo baada ya mtanange huo kumalizika.
 Kipa wa Simba Juma Kaseja, akipita jukwaani kupokea zawadi ya mshindi wa pili. 
 Baada ya kumalizika wachezaji wa Simba tu, Umemem ukazimika uwanja mzima, kilichofuata ni mashabiki kumuka kwa kutumia simu zao za tochi kama unavyoona jukwaani vimwekumweku vikitawala ndani ya giza nene.
 Ilibidi liitwe gari la Msaraba Mwekundu ili kutoa msaada wa kuwasha taa zake ili kumulika jukwaani hapo zoezi la utoaji tuzi na Kombe uendelee.....
 Hatimaye wachezaji wa Yanga walikabidhiwa Kombe lao wakaanza shangwe.....zisizo na kikomo..
 Mdau angalia kichwa hiki cha Kiiza ndilo lilikuwa goli la kwanza lililokataliwa eti ni Off side, je mpigaji huyu kweli alikuwa Off Side???......
 Hii ndiyo hasa iliyokuwa Krosi ya goli ikipigwa na Rashid Gumbo na goli likafungwa na Keneth Asamoh, huku Ulimboka akibaki kumshangaa Gumbo....
Picha ya juu ni baada ya Krosi, ilitua kichwani kwa Asamoh kama unavyomuona akijikunja, hapa tayari ameshapiga kichwa mpira huo sasa ukielekea langoni mwa Simba huku wachezaji wa simba wakiushangaa......Bango hili lililopo Makumbusho jana lilipata wateja wengi kuliko siku zote zilizopita baada ya mchezo huo kumalizika.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.