TIMU ya Yanga ya Dar es Salaam leo imeafanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Kagame kwa mbinde baada ya kumaliza dakika 90 kufungana na timu ya
Red Sea ya Eritrea na hatimaye kubebwa na penati katika mchezo uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini.
Yanga iliyokuwa na nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo, ilionekana kushindwa kuwamudu vyema waeritrea hao ambao walikuwa wakifanya mashambulizi yao kwa kushtukiza huku wanayanga nao wakipoteza nafasi kadhaa za magoli, jambo lililowafanya kufika hatua ya matuta.
Kwa hatua hiyo sasa Yanga watakutana na St.George ya Ethiopia ambayo nayo imetinga katika hatua hiyo ya nusu fainali baadaya kuitoa Vital’O ya Burundi kwa mabao 2-0, katika mechi ya kwanza ya robo fainali iliyopigwa leo mchana.
Baada ya Kigi Makasi kuwanyongonyesha Mashabiki wa Yanga kwa kukosa penati ya tatu katika hatua hiyo, hatimaye Nurdin Bakar,aliweza kuwainua mashabiki lukuki wa Yanga baada ya kufunga penati ya mwisho ambayo ilikuwa na kila hari ya kuwa na presha kwa mpigaji hadi mashabiki na wachezaji wote.
Ambapo pia kipa wa Yanga, Yaw Berko naye alionyesha umahiri wake na kuwakuna mashabiki pale alipopangua mkwaju mmoja kati ya saba ya Red Sea na kufanya Yanga kuibuka na ushindi wa 6-5.
No comments:
Post a Comment