Habari za Punde

*YANGA YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA KAGAME

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, jan  imejihakikishia kutinga  hatua ya robo fainali ya Michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, 'Kagame Cup', baada ya kuisambaratisha timu ya Bunamwaya ya Uganda kwa jumla ya magoli 3 - 2, katika mchezo wa kundi B uliochezwa katika Uwanja wa Taifa.
Beki wa Young Africans, Shadrack Nsajigwa, akimtoka beki wa Bunamwaya ya Uganda, wakati wa mchezo huo.

Yanga imetingab robo fainali baada kufikisha jumla ya pointi 7 huku ikifuatiwa na Bunamwaya yenye pointi 6 mbali na kukubali kipigo hicho nayo itakuwa nyuma ya mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara katika hatua ya robo fainali hizo.

Al Mereikh yaitwanga Elman

Katika mchezo mwingine uliochezwa katika uwanja huo huo wa Taifa Dar es Salaam Al Mereikh ya Sudan imesambaratisha Elman ya Sudan kwa jumla ya magoli 3 - 0. Japo Al Mereikh imeshinda mechi ya leo lakini itabidi kusubiri hadi mwisho ili kujua kama inaweza kupendekezwa kucheza hatua ya robo fainali kama matokeo yake yatakuwa ni mazuri kuliko timu nyingine zilizokosa kuingia hatua ya robo fainali.

St.George yaichukiza Port
Nako katika uwanja wa Jamuhuri uliopo mkoani Morogoro timu ya St. George ya Ethiopia leo imeinyeshea mvua ya magoli timu Port ya Djibout kwa kuitandika bila huruma magoli 7 - 0 katika mechi ya kundi C na hivyo kuingia moja kwa moja hatua ya Robo fainali ya mashindano ya CECAFA, Kagame Cup.

Ulinzi
Mbali na St.George timu nyingine iliyojihakikishia kuingia hatua ya robo fainali kutoka kundi C ni Ulinzi ya Kenya ambayo leo imecheza na APR na matokeo yalikuwa sare ya 0-0.

Simba V/S Red Sea 
Leo Jumapili kuna mechi mbili za kundi A kumalizia hatua ya makundi ambapo Simba ya Tanzania itacheza na Red Sea ya Eritrea na mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Zanzibar Ocean View na Vital'o ya Burundi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.