(48) mkazi kitongoji cha Kantalamba anashikiliwa na polisi kwa tuhuma
ya kumuua mkewe kwa kipigo kutokana kile kilichoelezwa ni wivu wa
kimapenzi.
Taarifa za polisi mkoa wa Rukwa, zinasema kuwa tukio la kuuawa kwa
mwanamke huyo aitwaye Tuli Mwakibinga (38) ambaye mhudumu wa afya
Habari zinadai kuwa mke huyo wa Katibu mwenezi wa CCM wa mkoa
lifikishwa hospitalini hapo akitokea hospitali teule ya Manispaa ya
Dk. Atman kwa ajili ya kupata matibabu baada ya kupigwa na kuumizwa
vibaya sehemu mbalimbali mwili wake ikiwamo kichwani.
Inadaiwa kuwa kabla ya kutokea kwa tukio hilo, juzi usiku nyakati za
saa 4, Katibu huyo alipata taarifa kwamba mkewe yupo kwenye moja ya
baa ya mjini hapa ambapo alimfuata na kumpeleka nyumbani kwa mwanamke
eneo la kristu mfalme ambako walianza mzozo akimtuhumu kuwa na
mahusiano na mwanaume mwingine ndipo walipoanza kupigana.
Inasemekana kwamba Maufi alimshambulia na kumuumiza vibaya kichwani
mwanamke huyo katika ugumvi uliodumu kwa muda mrefu hali
iliyosababisha kupata majeraha yaliyosababishwa kuanza kutokwa na
damu nyingi hadi alipookolewa na majirani waliosikia akipiga kelele za
kuomba msaada.
Majirani walioshuhudia tukio hilo walieleza kuwa walimchukua mwanamke
huyo na kumkimbiza hospitali ya Dk. Atman ili apate matibabu lakini
hali ilikuwa mbaya zaidi ambapo nyakati za saa 2:30 asubuhi ya jana
ambapo alipelekwa hospitali ya rufaa mjini hapa akiwa amepoteza fahamu
na kulazwa hodi ya wagonjwa mahututi lakini alifariki dunia muda mfupi
baadaye.
Mganga mkuu wa mkoa, Dk. Sadun Kabuma alithibitisha kutokea kwa kifo
hicho na kueleza kuwa baada ya uchunguzi wa kitatibu imebainika kuwa
alifariki dunia kutokana kuvuja damu nyingi ndani ya ubongo na shingo
yake ilikuwa imevunjika.
“inawezekana kuwa muuaji alikuwa akikibamiza kichwa cha marehemu
ukutani kwa nguvu hali iliyosababisha kuvuja kwa damu nyingi kwenye
ubongo wake...... hata hivi navyozungumza na wewe baada ya saa kadhaa
kupita marehemu huyo bado anaendelea kuvuja damu puani” alisema Dk.
Kabuma
Naye Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa, Isuto Mantage alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kuongeza polisi inamshikili Katibu huyo wa
CCM na atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi wa awali
kukamilika.
No comments:
Post a Comment