Habari za Punde

*MKUTANO WA 20 WA MAGAVANA WA ACBF WAANZA ARUSHA


Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha, Ngosha Said Magonya, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa 20 wa Bodi ya Magavana wa Afrika (ACBF) kwa niaba ya Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo, jijini Arusha jana. Picha za Vicent Tiganya-MAELEZO
Profesa Samwel Wangwe (kushoto) na Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha Ngosha Said Magonya, wakibadilishana mawazo wakati wa mkutano wa 20 wa Bodi ya Magavana ulioanza jana jijini Arusha, ambao utafunguliwa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal kesho.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 20 wa Bodi ya Magavana wa Afrika (ACBF) wakifuatilia mijadala mbalimbali wakati wa mkutano huo ulioanza jana  Arusha.
Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana wa Afrika (ACBF) na pia aliyewahi kuwa Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Sten Rylander (kushoto) akiwa na Kamishna wa Fedha za Nje wa Tanzania Ngosha Said Magonya (wa pili kushoto), Waziri Mkuu Mstaafu wa Mauritania, Zeine Ould Zeidaneb(wa pili kulia) na Katibu Mtendaji wa ACBF Dkt Franniel Leautier (kulia) wakati wa mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.