Wadau wakimsaidia Mzee Kipara nyumbani kwake wakati walipofika kumjulia hali. |
Mzee Kipara wa enzi za Mchezo wa redio na miaka ya karibuni katika kundi la maigizo la Kaole Sanaa Group, Je Wasanii mpo wapi kwa suala hili la kumsaidia msanii mwenzenu Nguli na mwalimu katika tasnia ya maigizo?
Mtandao huu pamoja na Global Publishers kupitia mwandishi wake tunapenda kuwawashukuru wadau wote walioshiriki kuweza kutoa taarifa hizi za Mzee kipara, hasa zaidi wana Blog wote kwa kuweza kuwajuza watanzania wote hali ya Msanii huyu maarufu mkongwe wa Maigizo.
Mimi binafsi kama mmiliki wa mtandao wa Sufianimafoto, Blog nawashukuru sana wana habari wa na Mabroger wote pamoja na Global Publisher kwa kutujuza juu ya suala hili ambalo wengi wetu hatukulifahamu.
Nawaomba Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo waweze kumsaidia huyu mzee, tuliowengi tunajua huyu Mzee Kipara alilitumikia Shirika la Utangazaji RTD enzi hizo na sasa TBC kwa kipindi kirefu, kwa hiyo ni vyema nao wakaliona hili, nalo pia ni la kwao si kwa wasanii peke yao.
Napenda nimuombe Mh. E. Nchimbi alitazame hili kwa umakini, tusimjali msanii pindi pale tunapomtumia bali hata katika wakati kama huu.
Tunawashukuru wenzetu wa Global Publishers kwa kumpatia simu ya mkononi Mzee huyu ambayo imesajiliwa na M-PESA, kwa hiyo kama umeguswa na hali yake na utapenda kumtumia kiasi chochote, unaweza ukawasiliana nae kwa namba:
+255 753 92 34
Mzee Kipara enzi zake wakati akiigiza na kundi la Kaole. |
No comments:
Post a Comment