Askari wa Usalama Barabarani, wakizungumza na dereva na abiria waliokuwa katika gari aina ya Suzuki yenye namba za Usajiri Z 484 DC, baada ya kuikamata maeneo ya Tunguu mjini Zanziba, hivi karibuni ikiwa imejaza mzigo ulioizidi uwezo na abiria huku ikipita katika barabara inayotumiwa na magari mbalimbali, jambo ambalo linaweza kusababisha ajali. Lakini baada ya askari hao kulikamata gari hili 'Stori; zilitawala zaidi kuliko kazi jambo lililoifanya kamera ya Sufianimafoto kushindwa kujua mwisho wa kamata hii ilikuwaje na kuamua kuondoka maeneo hayo na kuwaacha wakiendelea na stori huku wakilizunguka gari hilo kila kona.
DC Mpogolo Awapongeza Walimu kwa Kazi Kubwa ya Kuandaa Viongozi
-
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amewapongeza walimu kwa kazi kubwa
wanayoifanya katika jamii, akisema ni nguzo muhimu katika ujenzi wa taifa
...
5 days ago

No comments:
Post a Comment