Habari za Punde

*JUMUIA YA WATANZANIA WAISHIO MAREKANI WAMUAGA MAMA ASHA-ROSE MIGIRO KWA BONGE LA PATI JIJINI NEW YORK

Aliyekua msaidizi wa Katibu Mkuu wa UN Mh.Mama Rose Migiro akizungumza machache na Viongozi wa Jumuia ya Watanzania jijini New York katika Hafla maalum iliyoandaliwa na uongozi huo ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kutumikia Umoja wa Mataifa.

Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.
 Mh, Asha-Rose Migiro anarudi nyumbani Tanzania baada ya kuitumikia UN kwa kipindi cha miaka 5. 

 Mh Asha-Rose ni Mtanzania wa kwanza mwanamke kupata nafasi kubwa ya kufanya kazi katika Umoja wa Mataifa akiwa kama msaidizi wa Katibu Mkuu Ban Ki-Moon. 

Mh, Asha-Rose aliandaliwa hafla hiyo na uongozi wa Jumuia ya Watanzania hapa New York kama shukrani zao kwake ambaye alikuwa kama mlezi wa jumuia na alishirikiana na uongozi kwa hali na mali kila alipopata nafasi ya kufanya hivyo.

 Uongozi wa jumuia ya Watanzania New York unamtakia kila la kheri huko aendako na unategemea kuendelea kuwasiliana na kama mlezi.



  
Mama Asha Rose, akiongoza watanzania kuanza kujisevia...
Mama Asha-Rose Migiro akiwa na Shabani Mseba katibu wa Jumia ya Watanzania New York.
Kutoka kushoto Mwenyekiti wa Jumuia ya Watanzania New York Haji Hamisi, Balozi Manongi ambaye ni Msaidizi wa Mama Asha Rose, Shabani Mseba ambaye ni Katibu wa jumuia ya Watanzania New York na Mzee Temba mweka hazina wa jumuia ya watanzania New York.
Bwana Chiume akiwa na Mama Asha Rose Migiro.
Ukodak Moment na Mama Asha Rose.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Watanzania New York, Haji Hamisi, akiwa na Mama Asha-Rose Migiro
NY Ebra wa Vijithings akiwa na Mama Asha-Rose Migiro


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.