Habari za Punde

*RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAPISHA MAJAJI WAWILI NA KAMISHNA WA MAHAKAMA LEO

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Mhe. Edward Rutakangwa, kuwa kamishna  wa Tume ya Utumishi wa Mahakama katika hafla fupi iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Mh. Semistocles Kaijage (kulia) kuwa jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kabla ya uteuzi huo Mh. Semistocles Kaijage alikuwa jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam.
Jaji wa mahakama ya Rufaa Mh. Semistocles Kaijage, akifanya mahojiano na wanahabari baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam. Jaji Kaijage, amesema atahakikisha kuwa anatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria na kupunguza mlundikano wa kesi na kuhakikisha kuwa maamuzi yanatolewa kwa haki.
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Katibu Mkuu Kiongozi, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohammed Chande Othman, na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya hafla hiyo.
 Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na wanafamilia wa Jaji wa mahakama ya Rufaa Mh. Semistocles Kaijage.
Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na wanafamilia wa Jaji wa mahakama ya Rufani Mh. Mussa Kipenka.
Jaji wa mahakama ya Rufani Mh. Mussa Kipenka akisaini hati ya kiapo baada ya kuapishwa na Rais  Dkt. Jakaya kikwete leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Jaji mkuu wa Tanzania Mohammed Chande Othman.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.