Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Dkt. Diodorus Kamala (kulia) akizungumza na wanajumuiya ya Uingereza-Tanzania, wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa The Royal Commonwealth Club, jijini London, jana.
*****************
Jumuiya ya Uingereza- Tanzania ( BRITAIN- TANZANIA SOCIETY) jana iliandaa hafla fupi ya kusherekea miaka 50 ya Utaifa kati ya Nchi ya Uingereza na Tanzania, iliyofanyika katika ukumbi wa The Royal Commonwealth Club, jijini London.
Katika hafla hiyo wageni mbalimbali pamoja na wanachama walijitokeza kwa wingi na kujumuika kwa pamoja kuhudhuria hafla hiyo fupi ilioandaliwa kwa ajili ya kuchangia nchi ya Tanzania.
Miongoni mwa wageni waliohudhuria ni pamoja na balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Peter Kallaghe, pamoja na mkewe Mama balozi Joyce Kallaghe, Mwenyekiti wa Britain- Tanzania Society William Fulton JP DL.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Balozi wa Ubelgiji Mhe. Dkt. Diodorus Kamala, aliyetoa mada maalum kuhusu mafanikio, maendeleo na changamoto katika nchi ya Tanzania na jumuiya nzima ya Afrika mashariki.
Aidha Dkt. Kamala, alifafanua jinsi uchumi wa Tanzania unavyokua kwa kasi kutokana na takwimu kutoka Benki ya Dunia ambapo pia aliongelea kuhusu masuala ya utalii, mioundo mbinu, hali ya amani na usalama ambazo zimepelekea wawekezaji wengi kuwekeza katika nchi ya Tanzania.
Nchi ya Uingereza ndio nchi pekee inayoongoza katika uwekezaji katika nchi ya Tanzania Ikifuatiwa na India pamoja na Kenya.
Aidha Dkt. Kamala, aliwashukuru wana jumuiya wa Uingereza- Tanzania kwa kuendelea kuisaidia Tanzania kwa hali na mali ili kupambana na hali ya umaskini.
Baada ya kutoa mada yake kulikuwa na kipindi kifupi cha maswali na majibu kutoka kwa wanajumuiya pamoja na wadau waliohudhuria.
Nae mwenyekiti wa Computer 4 Afrika ndg Aseri Katanga, alitoa risala fupi ya kumshukuru mgeni rasmi kwa kujitolea kwake kuja kujumuika na wanajumuiya pamoja na hotuba yake nzuri kuhusu Tanzania.
Vile vile halfa hii ilijumuisha uoneshwaji wa picha zilizochorwa na wachoraji kutoka Tanzania ambazo zilinadiwa ili kuchangisha pesa za kuwasaidia kuwainua wadau wa tasnia ya uchoraji Tanzania.
Baadhi ya wachoraji ambao picha zao zilionyeshwa ni Mmadi Ausiy, Haji Chilonga, Hassan Kadudu, Florian Ludovick Kaija, James Haule na Aggrey Mwasha.
Wadau wa Jumuiya hiyo, waliohudhuria hafla hiyo....
Wanajumuiya hiyo wakipozi kwa picha kushoo love.....
![]() |
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, ambaye pia alikuwa meni rasmi katika hafla hiyo, Dkt. Deodorus Kamala (kulia) akipozi kwa picha na wadau wa Jumuiya hiyo, Frank Eyembe (katikati) na .......
|
Miongoni mwa picha zilizoonyeshwa na kunadiwa katika hafla hiyo...

.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
No comments:
Post a Comment