Bondia Fransic Cheka, akipima uzito kwa ajili yamaandalizi yA pambano lake na Kalama Nyilawila linalotarajia kufanyika siku ya jumamosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam.
Bondia Kalama Nyilawila, akipima uzito kwa ajili ya maandalizi ya pambano lake na Fransic Cheka litakalofanyika siku ya jumamosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam.
************************************
BAADA ya tambo za muda mrefu kati ya Kalama Nyilawila na Francis Cheka, na kutambiana kila mmoja akimtamani mwenzake na kuomba kila kukicha pambano, hatimaye siku ya kujua nani mbabe kati yao imetimia ambapo kesho, wababe hao watapanda Ulingoni katika Ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mabondia hao awali walishawahi kupigana katika pambano ambalo pia lilikuwa na upinzani mkubwa lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro na kumalizika kwa utata, baada ya Cheka kupewa ushindi wa Pointi na kuwafanya mashabiki wa mabondia hao kuunda uhasama baina yao na kuwa wakitafutana hadi mitaani kwa muda mrefu.
Akizungumza na mtandao huu jijini, Dar es Salaam jana, promota wa pambano hilo Oswald Mlay, alisema pambano hilo la raundi 12 la uzito wa Kg 72, litapigwa katika uwanja wa PTA Sabasaba.
Katika Mchezo huo kutakua na Uhuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.
Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi.
No comments:
Post a Comment