Habari za Punde

*SUMA LEE, MPOTO NA LINEX WAWAPAGAWISHA VILIVYO WAKATI WA BAGAMOYO

NA MAGRETH    KINABO- MAELEZO BAGAMOYO

.
MSANII  maarufu kwa jina la Mrisho  Mpoto(mjomba ) jana usiku alikonga nyoyo za   wakazi wa mji wa Bagamoyo  kwa kutoa burudani za nyimbo na mashairi.


Hali hiyo ilijitokeza  wakati wa Tamasha la 31  Sanaa na Utamaduni  linaloendelea katika Ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni(Tasuba), iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani.

 Msanii alipoingiajukwaa ni na kundi lake wakazi hao walionekana kumshangilia na wengine kusimama jukwaani na kucheza mara tu wimbo wake wa nyoosha kidole Adela ulipopigwa   na kuanza kugani mashairi yenye ujumbe mbalimbali.

Mpoto  kabla ya kupanda jukwaani alisindikizwa na wasanii wengine wawili wajulikanao kwa majina ya Suma Lee na Linex.

Wasanii hao waliwapagawisha wakazi hao  walipoimba nyimbo  mbalimbali mfano hakunaga.

Suma Lee alishangiliwa na wakazi hao pale alipoimba nyimbo ya Mpenzi naomba unipe nafasi, wakati Linex alifurahisha wakazi hao alipotamba na nyimbo ya Kigoma.
  
Wasanii hao pia wanampango wa kuzindua album mpya ijulikanayo kwa jina la Boda boda Oktoba 5, mwaka katika ukumbi huo.

Katika tamasha hilo pia kikundi vya ngoma, cha  Amani nacho kilifanya ukumbi ukiwa umetulia baada kuonesha ngoma kwa kucheza mitindo mbalimbali.

WAKATI HUO HUO:

WASANII wamepewa changamoto ya kujitokeza kwa wingi katika kutoa maoni juu ya uundaji wa  Katiba mpya ili fani yao iweze kutambulika  kisheria.
Kauli hiyo imetolewa  jana na Mkurugenzi  Idara ya Mfuko wa Uwezeshaji wa Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA), Charles Malimba   wakati akitoa mada   kuhusu  Sanaa ya  Utamaduni na dhana ya Tasnia ya Ubunifu inavyoweza kuleta ajira kwa vijana wa Tanzania katika Tamasha la 31 la Sanaa na Utamaduni linaloendelea   kwenye uwanja wa Taasisi  ya Sanaa na Utamaduni(Tasuba), Bagamoyo, mkoani Pwani.
Alisema kuna haja ya wasanii kujitokeza katika kutoa maoni juu ya Katiba mpya ili itambuena kutoa kipaumbele mambo mbalimbali katika sekta ya sanaa na utamaduni.
Aidha Malimba aliongeza kuwa wakati umefika kuwa Katiba itamke sanaa na utamaduni kazi , pia kuwepo na viwango vya malipo kisheria kwa kuwa  sekta hiyo inavyoweza kuchangia mapato kwa  serikali.
Malimba  alitaka vyuo vinavyofundisha sanaa utamaduni nchini  kutunza kumbukumbu za  fani  hizo na kuurithisha  ili kuepusha kupotea kwa utamaduni wa Mtanzania , huku akiwataka  wanafunzi wa fani hizo kusoma kwa bidii na kuitekeleza  ili kuweza kuwasaidia wengine na kuifanya sekta hiyo kuwa ajira.
Naye mhitimu wa chuo hicho wa mwaka 2010, Nyenyembe Jacoub na Baraka  Matitu walisema  ili kuweza kukuza sanaa na utamaduni kuna umuhimu  wa kuanzisha shule maalum  kuanzia chekechea hadi elimu ya juu.
Akijibu hoja hiyo, Malimba alisema ni changamoto kwa wadau mbalimbali  binafsi kuanzisha shule hizo kama ilivyo kwa zingine kwa kuwa suala hilo halina kipingamizi, huku akisisitiza suala la utunzaji wa sanaa na utamaduni ni wajibu wa kila wanajamii.  
Baadhi ya wasanii waliomba serikali iweke mikakati ya kuweza kuwasaidia wasanii hususan wale wachanga ili kuweza kukuza vipaji vyao, kwa kuwa vingi vinaanzishwa lakini vinashindwa kuendelea kwa kukosa wafadhili.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.