Habari za Punde

*HAMAD RASHID AUTAKA UMOJA WA MATAIFA KUFANYA KAZI KWA UKARIBU NA MABUNGE DUNIANI ILI KUTATUA MIGOGORO

 Mhe. Hamad Rashid Mohamed akitoa mchango wake katika Mkutano wa wa siku mbili wa masikilizano baina ya Mabunge duniani (IPU) na Umoja wa Mataifa kujadili namna bora ya Mabunge yote duniani kushirikishwa katika njia za kuzuia migogoro, usuluhishi pamoja na namna bora ya kujenga amani duniani uliofanyika Mjini New York Marekani na kumalizika leo.
 Mhe. Hamad Rashid Mohamed akifurahia jambo na baadhi ya wabunge wa kamati ndogo ya wabunge kutoka Tanzania, Uingereza na Pakistani iliyoundwa wakati wa Mkutano masikilizano baina ya Mabunge duniani (IPU) na Umoja wa Mataifa kuangalia namna bora ya Mabunge kuyawajibisha Mashirika ya Kimatifa kutokana na kuingilia migogoro yenye uvunjifu wa Amani Duniani katika mkutano wa ushirikishwaji wa Mabunge katika njia za kuzuia migogoro, usuluhishi pamoja na namna bora ya kujenga amani duniani uliofanyika Mjini New York Marekani na kumalizika leo.
 Senator wa Bunge la Pakistani Mhe. Mohammad Mohsin Khan Leghari akitoa mapendekezo ya kamati ndogo ya wabunge kutoka Tanzania, Uingereza na Pakistani iliyoundwa wakati wa Mkutano masikilizano baina ya Mabunge duniani (IPU) na Umoja wa Mataifa kuangalia namna bora ya Mabunge kuyawajibisha Mashirika ya Kimatifa kutokana na kuingilia migogoro yenye uvunjifu wa Amani Duniani katika mkutano wa ushirikishwaji wa Mabunge katika njia za kuzuia migogoro, usuluhishi pamoja na namna bora ya kujenga amani duniani uliofanyika Mjini New York Marekani na kumalizika leo. Kulia kwake ni Mhe. Hamad Rashi Mohamed na Mhe. Craig Whittaker kutoka Bunge la Uingereza.
Katibu Mkuu wa IPU Anders Johnson akimpongeza Mhe. Hamad Rashi Mohamed kwa mchango wake uliosisimua mkutono huo mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa namna bora ya kushirikisha Mabunge yote duniani kushiriki katika njia za kuzuia migogoro, usuluhishi wake pamoja na namna bora ya kujenga amani duniani uliofanyika Mjini New York Marekani kwa siku mbili na kumalizika leo. Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.