Hoteli ya kitalii Ikondolelo Lodge iliyoko Kibamba Jijini Dar es salaam , Imeteuliwa na Bodi ya mashindano ya Miss Utalii Tanzania kuwa Kambi rasmi ya mashindano hayo ya Mwaka huu 2012.
Mchakato wa uteuzi ulihusisha Hotel zaidi ya saba zilizojitokeza kudhamini fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2012.
Hotel ya Ikondolelo kuwa Kambi ya Miss utalii Tanzania itatumia zaidi ya Shilingi za kitanzania Milioni 100, ikiwa ni udhamini wa gharama za kambi ya Warembo na waandaaji zaidi ya sitini (60) kwa muda wa wiki tatu.
Bodi katika kuteua hotel rasmi ya mashindano mwaka huu imezingatia Vigezo vifuatavyo: Usalama wa watu na mali zao, ubora wa viwango vya huduma ambayo siyo chini ya hadhi ya nyota (3) , mazingira a hotel na utulivu wa eneo husika kulingana na viwango vya kitaifa na Kimataifa vya mashindano ya Miss Utalii,pia kwa kuzingatia viwango vilivyo wekwa na serikali kupitia Baraza la sanaa la Taifa (BASATA).
Warembo kutoka mikoa yote ya Tanzania na Vyuo vikuu , wakiwa kambini katika Hotel ya Ikondolelo watafanya shughuli mbalimbali za maandalizi na za kijamii; zikiwemo , Kujifunza kuogelea katika bwawa lililopo hotelini hapo, Upigaji wa piga za minato katika bustani zinazo zunguka hoteli, watapewa mafunzo maalum ya kutumia maeneo na vifaa mbalimbali vya hotel za kitalii. Aidha washiriki wa fainali za taifa za Miss utalii 2012 watapewa mafunzo kuhusiana na utalii, utamaduni, uwekezaji, mazingira,afya ya jamii,elimu ya jamii uzalendo,watafundishwa mbinu za kujieleza, kujiamini na kufanya matangazo.
Mkurugenzi mtendaji wa Ikondolelo Lodge Ndugu Fredy Selekwa ameishukuru Bodi ya Miss utalii Tanzania kwa kuwapa fulsa ya kuwa hotel Rasmi ya Mashindano haya muhimu kwa taifa katika kukuza secta ya utalii na uchumi kwa ujumla. Ameihakikishia washiriki na viongozi watakao kuwa kambini kuwapatia huduma zote muhimu kwa kiwango cha kimataifa
Imetolewa na
Hamisi .A. Mkongowale
Mratibu wa Matukio
No comments:
Post a Comment