Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Ngosi Mwihava, akifungua mafunzo kwa watendaji kutoka taasisi za utafiti wa vyakula na magonjwa ya binadamu kuhusu athari zinazoweza kujitokeza kutokana na bioteknolojia ya kisasa. Mafunzo hayo yamefanyika leo katika Hoteli ya Giraffe Ocean View, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Washiriki wa warsha ya Tathmini ya athari zinazoweza kujitokeza kutokana na teknolojia za kisasa wakifuatilia mafunzo yanayotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais – Idara ya mazingira. Mafunzo hayo yanaendelea katika Hotel ya Giraffe Ocean View, jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Ngosi Mwihava (kulia) akibadilishana mawazo na Dk. Flora Ismail kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Dk. Julius Ningu, Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais mara baada ya kufungua mafunzo kwa watendaji kutoka taasisi za utafiti wa vyakula na magonjwa ya binadamu kuhusu athari zinazoweza kujitokeza kutokana na bioteknolojia ya uhandisi jeni.
Washiriki wa mafunzo ya Tathmini ya athari zinazoweza kujitokeza kutokana na bioteknolojia za kisasa wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Ngosi Mwihava (wa tatu kutoka kulia) mara baada ya kufungua mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment